Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe awakaribisha Dk. Slaa, Mwabukusi Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe awakaribisha Dk. Slaa, Mwabukusi Chadema

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe, amemkaribisha aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbroad Slaa, arejee baada ya kutimkia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mbali na Dk. Slaa, leo tarehe 15 Februari 2024 katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, Mbowe alimkaribisha wakili machachari Boniface Mwabukusi ajiunge na chama hicho, akisema Chadema hakina adui wa kudumu bali kinachodumu kwake ni maslahi ya nchi.

“Leo Chadema tunasimama kama chama kikuu cha upinzani kwa sababu kuna watu wametoa damu na jasho kuifanya Chadema tunajivunia leo ifike mahali hapa. Sisi ndani ya Chadema hatuna tumesema hatuna adui wa kudumu au rafiki wa kudumu ila ambacho cha kudumu ni maslahi ya nchi yetu ndio maana kwenye jukwaa hili nafurahi kumtambulisha katibu mkuu wangu wa zamani Dk. Slaa,” amesema Mbowe.

Amesema “Dk. Slaa ameshughulika kukijenga , kama yuko tayari tufanye kazi pamoja, karibu katibu mkuu Chadema chama chako tunahitaji wote tushirikiane. Unamuona ndugu yangu Mwabkusi leo wako hapa wanatambulisha sauti ya watanzania, lakini wote ni zao la Chadema karibuni nafasi yenu bado ipo.”

Dk. Slaa aliyetimkia CCM akipinga ujio aliyekuwa mgombea urais wa Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Edward Lowassa, amekaribishwa na Mbowe baada ya kushiriki maandamano ya amani yaliyoandaliwa na chama hicho kudai katiba mpya na kupinga ugumu wa maisha.

Mwanasiasa huyo mkongwe alishiriki maandamano hayo akiwa na Mwabukusi, wakiwakilisha kikundi chao cha Sauti ya Watanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!