July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yashauriwa kuanzisha mitaala elimu ya anga shule za sekondari

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imeshauriwa kuanzisha mtaala wa elimu kuhusu usafiri wa anga, kwa shule za sekondari hadi kidato cha sita, ili kutoa fursa kwa wanafaunzi wanaopenda kusomea masuala hayo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ushauri huo umetolewa leo Jumamosi, tarehe 21 Mei 2022  na Tunu Pinda, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, katika uzinduzi wa masomo ya usafiri wa anga kwenye Shule ya Sekondari Alpha, jijini Dar es Salaam.

Mama Tunu amesema, watoto wengi wamekuwa wakipenda kujihusisha na masuala ya usafiri wa anga, hasa urubani wa ndege, lakini ndoto zao zimekuwa zinaishia njiani kwa kuwa hakuna msingi unaowawezesha kufahamu zaidi masuala hayo.

“Lakini kuna wale ambao wanatamani sana lakini hawajui wanapata wapi, niiombe Serikali wawe na mtaala kwa ajili ya elimu ya anga. Kiwe kitu ambacho wanafunzi wanasoma wakiwa wadogo kuanzia kidato cha kwanza hadi sita ili kama ana ndoto ya kuwa rubani iweze kutimia,” amesema Mama Tunu.

Aidha, Mama Tunu ameupongeza uongozi wa Shule za Alpha, kwa kuanzisha masomo hayo licha ya kwamba bado hayatambuliki kisheria.

“Nimefurahi kama wenzetu wa Alpha wameona jambo jema sana kwa watoto wetu kuanza kusoma tangu wadogo. Kufahamu mambo ya anga hasa kuendesha ndege na utaratibu wake,” amesema Mama Pinda.

Mkurugenzi wa Shule za Alpha, Fatina Senzota, amesema masomo hayo yanatolewa kwa wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita, ambapo shule zake zinasaidiana na taasisi mbalimbali za kimataifa, ikiwemo Kenya School of Airline na Shirika la Ndege la Uturuki (Turkish Airline).

“Kuna makampuni tumebahatuka kujiunga nayo, ikiwemo Kenya School of Airline, ambapo watoto wakipata likizo wataenda Kenya kufanya mafunzo kwa vitenso na watapewa cheti. Pia tunashirikiana na Turkish Airline na watalaamu wao wako hapa, watoto watakaopenda wataenda wakati wa likizo Uturuki kujifunza,” amesema Fatina.

Fatina amesema, mafunzo hayo yanatolewa kwa wanafunzi wa micheouo yote, ikiwemo sayansi na sanaa.

error: Content is protected !!