Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yaokoa Bil. 236/- baada ya kushinda mashauri 451
Habari za Siasa

Serikali yaokoa Bil. 236/- baada ya kushinda mashauri 451

Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene
Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imeokoa kiasi cha Sh. 236.6 bilioni katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, baada ya kushinda mashauri ya madai 444 na ya usuluhishi saba. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa, tarehe 11 Machi 2022, jijini Dar es Salaam na Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene, akitaja mafanikio ya Serikali hiyo ya Awamu ya Sita, kuanzia Machi 2021 hadi Februari mwaka huu.

Simbachawene amesema, mafanikio hayo yametokana na wizara yake kupitia Ofisi wa Wakili Mkuu wa Serikali, kujenga uwezo wa kitaasisi katika kuratibu, kusimamia, na kuendesha mashauri ya madai na usuluhushi kwa kuzingatia maslahi ya Taifa.

“Katika kipindi husika, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, iliwakilisha Serikali na taasisi zake kwenye mashauri 1,391, kati ya hayo, mashauri ya madai yalikuwa 1,274 na ya usuluhishi 117. Mashauri ya madai yaliyomalizikia na kushinda ni 444 na usuluhishi yalikuwa 7,” amesema Simbachawene.

Simbachawene amesema “katika kushughulikia mashauri hayo, kiasi cha Sh. 236.6 bilioni zimeokolewa na Serikali kupata manufaa.”

Aidha, Simbachawene amesema katika kipindi hicho, Serikali iliifanya maboresho Sheria ya Usuluhishi sura ya 15 , kwa ajili ya kuimarisha mfumo wa utatuzi wa migogoro nje ya mahakama kwa kutumia njia ya maridhiano, upatanishi na usuluhishi, kwa lengo la utoaji haki kwa gharama nafuu.

Amesema kupitia marekebisho ya sheria hiyo, wizara yake imesajili na kuwapatia vyeti vya kufanya kazi, wasuluhishi 192, wapatanishi 106, waendesha majadiliano 37 na waendesha maridhiano 23.

“Kupitia sheria hizi, wizara imeweka utaratibu wa usajili na kuendelea kuwasajili, kuwatambua na kuwadhibiti wasuluhishi, wapatanishi, waendesha majadiliano na maridhiano ili kudhibiti maadili na mienendo yao,” amesema Simbachawene.

Katika hatua nyingine, Simbachawene amesema, katika kipindi hicho, uwezo wa usikilizwaji mashauri mahakamani umeongezeka kwa asilimia saba, kutoka asilimia 92 iliyokuwepo Machi 2021 hadi kufikia asilimia 99.

Amesema, kuanzia Machi 2021 hadi Februari 2022, yalifunguliwa mashauru 181,768, ambapo 180,162 yalisikilizwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!