Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yamkabidhi majukumu Spika Tulia kuhusu IPU
Habari za SiasaTangulizi

Serikali yamkabidhi majukumu Spika Tulia kuhusu IPU

Spika Dk. Tulia Ackson
Spread the love

SERIKALI imemtaka Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dk. Tulia Ackson, kutumia nafasi hiyo kuhakikisha analinda maslahi ya Tanzania katika jumuiya za kimataifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Maagizo hayo yametolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, leo tarehe 30 Oktoba 2023, katika hafla ya kumpokea Dk. Tulia ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania, iliyofanyika jijini Dodoma.

Waziri Majaliwa amesema, Serikali ina mikataba mingi iliyoingia katika Umoja wa Mataifa, hivyo inaamini Spika Tulia atatumia nafasi hiyo kupenyeza ajenda za Tanzania.

“Sisi tumefarijika kama Serikali, sababu moja kati ya majukumu yako kwamba utakuwa unahudhuria vikao vyote vya Umoja wa Mataifa na sote tunajua kwamba Serikali yetu tunayo mikataba yetu tuliyokuwa nayo kwenye Umoja wa mataifa,”

“ Sisi tunashukuru sababu tutakutumia utakapokuwa unaenda kwenye vikao kwa kuingiza ajenda za nchi. Tuna hakika utatupigania,” amesema Waziri Majaliwa.

Katika hatua nyingine, Waziri Majaliwa amesema viongozi wa nchi wanampongeza Spika Tulia kwa kushinda nafasi hiyo nyeti, akisema ameiheshimisha nchi  na mhimili anaouongoza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

error: Content is protected !!