SERIKALI imemaliza mgogoro wa ardhi kati ya Halmashauri ya Handeni na Kilindi, kwenye eneo la Bondo, uliodumu kwa miaka kadhaa. Anaripoti Jemimah Samwel, Dar es Salaam…(endelea).
Taarifa hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dk. Festo Dugange, leo tarehe 9 Novemba 2023, bungeni jijini Dodoma, akijibu swali la Mbunge wa Handeni Mjini, Reuben Kwagilwa (CCM) aliyehoji lini Serikali itamaliza mgogoro wa mpaka kati ya Handeni na Kilindi, ili kuepusha migogoro inayoendelea kila siku.
Dk. Dugange amesema mgogoro huo umemalizika kufuatia maelekzo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba, kwenye kikao kilichofanyika tarehe 23 Julai mwaka huu.
Katika hatua nyingine, Dk. Dugange amesema timu ya watalaam wa ardhi, wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya na viongozi wa wilaya hiyo, walikutana tarehe 8 na 9 Oktoba 2021, kwa ajili ya kupitia tangazo la Serikali la kuhakiki idadi ya watu na upatikanaji wa huduma za kijamii.
“Nitoe wito kwa mkurugenzi wa halmashaurikutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa uhifadhi wa misitu, kuheshimu mpaka ulioanishwa kutokana na tafsiri ya tangazo la serikali. kurekebisha usajiri wa shule za msingi Gondo na Kalakwio ili zisomeke ndani ya wilaya husika,”amesema Dk. Dugange.
Leave a comment