Sunday , 3 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Muhongo ataka Serikali ibuni miradi kufuta umaskini
Habari za Siasa

Muhongo ataka Serikali ibuni miradi kufuta umaskini

Prof. Sospeter Muhongo, Mbunge wa Musoma Vijijini
Spread the love

MBUNGE wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, ameshauri mipango mbalimbali inayowekwa na Serikali, ijielekeze katika utekelezaji miradi ya kufuta umasikini nchini. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Prof. Muhongo ametoa ushauri huo leo tarehe 9 Novemba 2023, bungeni jijini Dodoma, wakati anachangia mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali 2024/25 na mwongozo wa maandalizi ya mpango na bajeti ya Serikali kwa mwaka ujao wa fedha.

Mbunge huyo wa Musoma Vijijini mkoani Mara, amesema takwimu za hali ya umasikini nchini, zinaonyesha kwamba, asilimia 18.7 ya watanzania wako chini ya mstari wa matatizo ya chakula, huku asilimia 35.7 wakiwa chini ya mstari wa matumizi ya kawaida, huku hali ya umasikini kwa nchi nzima ni asilimia 13.

Prof. Muhongo amesema ili Serikali iweze kuondoa umasikini, inabidi iongeze nguvu katika sekta ya mifugo, madini, uvuvi, utalii na miundombinu ya barabara.

“Kwa hiyo mipango yetu ijielekeze kwenye miradi ya kufuta umasikini, ili uchumi wetu ukue kati ya asilimia nane hadi 10, kwanza tujielekezekwenye uchumi wa gesi tatu ikiwemo gesi asilimia na gesi nyingine. Tuwekeze katika madini, kilimo, uvuvi na utalii, hivi vyanzo vipaumbele vya mapato,” amesema Prof. Muhongo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko aagiza wakurugenzi TANESCO kukemea rushwa kwenye maeneo yao

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Tunastawisha ufisadi na kuchukia matunda yake

Spread the loveBUNGE la Jamhuri linaloendelea mjini Dodoma, kwa wiki nzima limetawaliwa...

error: Content is protected !!