Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yaanika mikakati upanuzi wa viwanja vya ndege Kigoma
Habari za Siasa

Serikali yaanika mikakati upanuzi wa viwanja vya ndege Kigoma

Uwanja wa ndege Kigoma
Spread the love

SERIKALI imesema itaendelea kujenga na kupanua miundombinu ya viwanja vya ndege ili kujihakikishia utoaji wa huduma ndani ya nchi na nchi jirani. Anaripoti Mwandishi wetu , Kigoma…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile wakati wa ziara yake katika uwanja wa ndege wa Kigoma ikiwa ni sehemu ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Viwanja vya ndege nchini (TAA).

Katika ziara hiyo, Kihenzile amekagua upanuzi wa njia ya kuruka na kutua ndege kwenye uwanja huo.

Awali, Meneja wa uwanja wa ndege wa Kigoma, Mbura Daniel amesema kwa sasa uwanja huo unahudumia abiria 33,0000 kwa mwezi na miruko 102 hadi 105 kwa mwezi.

Amefafanua kuwa katika safari sita za wiki, zinahusisha safari tatu za nje ya nchi hasa Burundi ambazo hufanywa na Shirika la Ndege la Taifa -ATCL.

Ameongeza kuwa upanuzi wa uwanja huo utahusisha njia ya kuruka na kutua ndege kutoka mita 1800 hadi 3000.

Pia, eneo la megesho ya ndege, mnara wa kuongozea na jengo la abiria huku ukitarajiwa kuhudumia abiria 400,000 kwa mwaka na kuwekewa taa za kuongozea ndege ili utumike kwa saa 24.

Amesema serikali inaithamini sekta ya uchukuzi kwa njia ya anga kama mishipa ya ukuzaji uchumi na shughuli mbalimbali za utoaji huduma kwa wananchi ndani na nje ya nchi.

“Ndiyo maana imewekeza fedha nyingi kwenye maboresho, ukarabati na upanuzi wa viwanja vyetu vya ndege na ununuzi wa ndege kwa ujumla.

“Uchukuzi kwa njia ya anga ni uchumi pia diplomasia, kadri unavyojenga na kuboresha viwanja vya ndege ndivyo unavyojenga ushawishi kwa jamii inayokuzunguka ndani na nje ya nchi,” amesema Kihenzile

Aidha, Kihenzile amewataka wakala wa barabara nchini Tanroads na menejimenti ya uwanja wa ndege wa Kigoma kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi kumaliza upanuzi huo kwa wakati na kiwango stahiki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!