JUMLA ya watu 13 wakiwamo wanawake sita na wanaume saba wamefariki dunia baada ya basi la kampuni ya Ally’s Star Bus kugonga kichwa cha treni chenye namba V951 90O06 kilichokuwa kikitokea Stesheni ya Aghondi kuelekea Manyoni katika makutano ya reli na barabara eneo la Manyoni mkoani Singida.
Basi hilo la abiria lenye namba za usajili T178 DVB mali ya kampuni ya Ally’s Star Bus limepata ajali alfajiri ya leo tarehe 29 Novemba 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC), Jamila Mbarouk imesema ajali hiyo imesababisha pia majeruhi 25.
“Ajall imehusisha basi la abiria lililokuwa likivuka njia ya reli eneo la Kilomita 587 Manyoni na kichwa cha treni na kusababisha majeruhi 25 kati yao wanawake saba, wanaume 18 na vifo vya watu 13 wanawake sita, wanaume saba.
“Shirika linaendelea kuwasihi madereva wa vyombo vya moto kufuata sheria na alama za usalama katika njia ya reli na barabarani zilizowekwa ili kuepusha ajali.
“Shirika linatoa pole kwa ndugu wa marehemu na Mwenyezi Mungu awape nafuu majeruhi waweze kuendelea na shughuli za kujenga taifa,” imesema taarifa hiyo.
Leave a comment