Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yaahidi kuunga mkono kampeni GGML KiliChallenge
Habari Mchanganyiko

Serikali yaahidi kuunga mkono kampeni GGML KiliChallenge

Spread the love

WAZIRI wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama amesema Serikali itaendelea kuunga mkono kampeni ya GGML KiliChallenge inayolenga kuchangisha fedha kwa ajili ya kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi kwani inalandana na jitihada za Serikali kutokomeza maambukizi mapya ya ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Pia amemwagiza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuhakikisha wanafunzi wawili wa miaka 14  waliopanda mlima Kilimanjaro kwa siku 7 kupitia kampeni hiyo iliyoasisiwa miaka 22 iliyopita kuingizwa kwenye orodha ya miongoni mwa watu watakaohudhuria sikukuu ya mashujaa ambayo itafanyika Julai 25 mwaka huu.

 

Mwanafunzi wa Shule ya msingi kivukoni, Rebecca Damian (14) akikabidhiwa cheti na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama (kushoto) baada ya kufika katika kilele cha Uhuru cha Mlima Kilimanjaro kuhamasisha uchangishaji wa fedha za mapambano dhidi ya VVU/Ukimwi kupitia kampeni ya GGML KiliChalenge -2023. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong.

Kampeni hiyo iliyoasisiwa na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (Tacaids) mwaka 2002 pia inalenga kuisaidia serikali kutimiza malengo ya kitaifa ya kufikia sifuri tatu – kutokuwa na maambukizi mapya, kutokuwa na unyanyapaa na ubaguzi, na kutokuwa na vifo vitokanavyo na Ukimwi.

Akizungumza katika hafla ya kuwapokea washiriki 35 waliopanda mlima Kilimanjaro na 26 waliouzunguka mlima huo kwa baiskeli mwishoni mwa wiki wilayani Moshi, Mhagama alisema GGML imeonesha kitendo cha kishujaa kuratibu kampeni hiyo kwa miaka zaidi ya 22.

“Kwa hiyo GGML kujitoa kubeba maumivu ya siku saba kwa ajili ya maumivu ya watanzania, hili jambo hili ni la kijasiri, la kishujaa litaendelea kukaa kwenye vitabu vya mambo ya msingi yaliyofanywa na taasisi zetu nchini. Kwa mfano huu mzuri uliooneshwa na GGML napenda kuwaambia hongereni sana,” alisema.

Alitoa wito kwa mashirika mengine ya kitanzania na ya kimataifa kuiga mfano wa GGML kuihudumia jamii kwa moyo wa dhati na kujitoa.

Mwanafunzi wa shule ya msingi Mbugani ambaye alirudia njiani baada ya kuugua malaria akiwa anapanda Mlima Kilimanjaro, Abel Musa(14) akikabidhiwa cheti na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama (kushoto).

Aidha, aliwapongeza washiriki pamoja na watoto hao waliopanda mlima tarehe 14 Julai mwaka huu na kushuka tarehe 20 Julai na kusisitiza kuwa ni mashujaa ambao mafanikio yao yamedhihirisha kuwa mwitikio dhidi ya VVU na Ukimwi unawezekana iwapo kutakuwa na dhamira ya dhati kwa kila Mtanzania kutokomeza janga hilo nchini.

Mmoja kati ya wanafunzi hao ambaye alifanikiwa kupanda mlima Kilimanjaro na kufika katika kilele cha uhuru ni Rebecca Damiani(14) mwanafunzi wa shule ya msingi Kivukoni na Abel Musa(14) mwanafunzi  wa shule ya msingi Mbugani ambaye alirudia njiani baada ya kuugua malaria akiwa mlimani.

Kiongozi wa washiriki waliozunguka mlima Kilimanjaro kwa baiskeli, Andrew Mazula akikabidhiwa cheti na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama (kushoto) baada ya kushiriki kampeni ya GGML KiliChallenge -2023 inayolenga kuhamasisha uchangishaji wa fedha za mapambano dhidi ya VVU/Ukimwi. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong.

Wanafunzio hao wanatoka katika Kituo cha kulea watoto wanaoshi katika mazingira magumu – Moyo wa Huruma- Geita ambacho kinafadhiliwa na GGML.

Mhagama alisema watoto hao wameonyesha uzalendo mkubwa kwa Taifa kwa  kujitosa kuungana na watanzania wengine katika kuchochea nguvu ya mapambano dhidi ya maambukizi mapya  ya virusi vya Ukimwi nakwambia wanapaswa kutambuliwa kama mashujaa katika nchi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama (katika) akiwa na baadhi ya washiriki wa kampeni ya GGML KiliChallenge -2023 inayolenga kuhamasisha uchangishaji wa fedha za mapambano dhidi ya VVU/Ukimwi.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong aliishukuru serikali kwa kuunga mkono katika mapambano hayo nakuhakikisha zinapatikana fedha kwa ajili ya kutokomeza janga la Ukimwi hapa nchini.

Waendesha baiskeli 26 walipanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuhamasisha uchangishaji wa fedha za kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/Ukimwi kupitia kampeni ya GGML KiliChalenge -2023.

Aidha, aliwapongeza watoto hao kwa rekodi ya kipekee waliyoiweka na kuahidi kuwa GGML itaendelea kuwaunga mkono katika kutimiza ndoto zao.

Washiriki 35 waliopanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuhamasisha uchangishaji wa fedha za kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/Ukimwi kupitia kampeni ya GGML KiliChalenge -2023.

Kaimu Mkurugenzi Tacaids, Jerome Kamwela  aliwapongeza wapanda mlima hao na kusema wamekuwa mabalozi wazuri katika kuendeleza mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi hapa nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

error: Content is protected !!