Saturday , 2 December 2023
Home Kitengo Biashara Serikali kununua mitambo 15 ya kuchoronga miamba
BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kununua mitambo 15 ya kuchoronga miamba

Spread the love

Serikali kupitia Wizara ya Madini imepanga kununua mitambo 15 ya uchorongaji wa miamba kwa ajili ya utafiti wa kina wa madini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita…(endelea).

Hayo yamebainishwa leo tarehe 25 Septemba 25 2023 na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde wakati akizungumza katika kipindi cha Jambo Tanzania (TBC1) kwenye maonesho  ya sita ya teknolojia ya madini yanayoendelea katika viwanja vya EPZ bomba mbili mkoani Geita.


Akielezea kuhusu mkakati wa  VISION 2030 Madini ni Maisha na Utajiri, Mavunde  amesema kuwa Serikali imejipanga kufanya utafiti wa Madini nchi nzima kwa lengo la kupata taarifa zitakazo weza kufungamanisha sekta ya madini na sekta nyingine za kiuchumi.

Akifafanua hali ya utafiti wa madini  amesema mpaka sasa utafiti wa kina umefanyika kwa asilimia 16 tu ambazo taarifa zake ndio zinatumika lengo  la Serikali ni kuongeza taarifa kupitia tafiti nyingine ziitakazofanywa na GST.

Mpaka sasa sekta ya madini inachangia asilimia 56 ya fedha za kigeni ambazo zinachangia asilimia 9.1 ya pato la Taifa(GDP) , hii ni kwa utafiti wa 16% uliofanyika , hivyo kufikia 2030 tutakuwa  tumefanya utafiti nchi nzima.

Sambamba na hapo Mavunde ameeleza kuwa Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira  zitaendeleza juhudi za kutunza mazingira kama Sheria zinavyoelekeza.

Pia Waziri Mavunde ameshiriki zoezi la upandaji miti katika viwanja vya maonesho vya EPZ.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Biashara

Shinda mtonyo mrefu ukicheza Shaolin Crew kasino ya  Meridianbet

Spread the love  TAIFA la Uchina limebebwa na historia kubwa sana, wengi...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mwalimu jela miaka mitatu kwa rushwa

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu...

Habari Mchanganyiko

Waziri Bashungwa aagiza wahandisi kujengewa uwezo

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Bodi ya Usajili wa...

error: Content is protected !!