Saturday , 2 December 2023
Home Kitengo Biashara Mtanzania aweka rekodi kimataifa kwa kiwanda cha kusafisha dhahabu
BiasharaHabari Mchanganyiko

Mtanzania aweka rekodi kimataifa kwa kiwanda cha kusafisha dhahabu

Mwekezaji Mtanzania, Sarah Masasi (kulia).
Spread the love

IMEELEZWA kuwa Kiwanda cha Kusafisha dhahabu cha Geita Gold Refinery (GGR) kinachomilikiwa na Mwekezaji Mtanzania, Sarah Masasi kimeiweka Tanzania katika Soko la Kimataifa katika usafishaji wa dhahabu duniani kutokana na ubora na uwezo wa kisafisha dhahabu tani 6000 kwa siku. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

 

Hayo yameelezwa  na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde leo tarehe 25 Septemba 2023 mkoani Geita baada ya kutembelea na kuzungumza na mwekezaji na wafanyakazi wa kiwanda cha kisasa cha kusafisha madini ya dhahabu cha GGR.

Mavunde amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kiwanda hicho kupata Ithibati ( ISO Certification) za aina tano ikilinganishwa na kiwanda kikubwa cha kusafisha madini ambacho hakina ISO zote hizo.

Pia, Waziri Mavunde ameiagiza timu ya wataalam iliyoundwa ikihusisha wataalam kutoka Benki Kuu ya Tanzania, Wizara ya Madini, wawakilishi wa wachimbaji wadogo na wamiliki wa viwanda vya usafishaji wa madini kuandaa taarifa itakayoelezea namna bora ya upatikanaji wa malighafi na ushiriki wa BoT kwenye kuwasaidia wachimbaji wadogo kuzalisha dhahabu itakayopelekwa kwenye viwanda hivyo.

“Dhahabu itakayosafishwa kwenye viwanda hivi sehemu ya uzalishaji huo itanunuliwa na Benki Kuu ya Tanzania,” amesema Mavunde.

Aidha, amesema kuwa ili kuwezesha kiwanda hicho kupata malighafi ya kutosha amemuagiza Katibu Mkuu, Wizara ya Madini kuitisha kikao na wadau wote wanaomiliki leseni za madini ili kuzungumza kwa pamoja na hatimaye  viwanda vya usafishaji madini ya dhahabu vya ndani ya nchini vipate malighafi ya kutosha.

Kwa upande wake, Mmiliki wa Kiwanda hicho cha Geita Gold Refinery (GGR) Mama Masasi ameishukuru  Serikali kwa kumpatia ushirikiano katika kipindi chote kuanzia ujenzi hadi kukamilika na kuanza usafishaji wa dhahabu katika ubora wa  999.9.

“GGR tupo tayari kufanya kazi na Wachimbaji wote wa madini ili kusafisha dhahabu yao katika kiwanda hiki kwa kuwa  kimekidhi vigezo  muhimu vya kimataifa,” amesema Mama Masasi

Naye, Mbunge wa Geita Mjini, Costantine Kanyasu (CCM) amesema kuwa anatamani kumuona mwekezaji huyo anafanikiwa katika kiwanda hicho na kusisitiza  Serikali iendelee kumpa ushirikiano katika shughuli zake.

Aidha, ameomba tafiti zifanyike zaidi ili wachimbaji wapate maeneo mengi ya kuchimba madini na hatimaye kiwanda hicho kiweze kupata mzigo kutoka kwa wachimbaji wa madini ili kuongezwa thamani.

Wengine walioshiriki ziara hiyo ni  Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali, Kamishna wa Madini Dk. AbdulRahman Mwanga Mwenyekiti  wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula na watendaji wengine wa Wizara ya Madini na Taasisi zake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Biashara

Shinda mtonyo mrefu ukicheza Shaolin Crew kasino ya  Meridianbet

Spread the love  TAIFA la Uchina limebebwa na historia kubwa sana, wengi...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mwalimu jela miaka mitatu kwa rushwa

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu...

Habari Mchanganyiko

Waziri Bashungwa aagiza wahandisi kujengewa uwezo

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Bodi ya Usajili wa...

error: Content is protected !!