Saturday , 2 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23
Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the love

MWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam, Felix Kamugisha, amebabainisha masuala sita yaliyofanyiwa kazi kupitia mpango kazi wa 2022/23. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Masuala hayo yamebainishwa Leo tarehe 2023, wakati ngome hiyo inazindua makala maalum inayoonyesha kazi ilizofanya katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu, tangu uongozi wake ulipochaguliwa Machi 2022.

Masuala yaliyotangazwa na Kamugisha ni, ufunguzi wa matawi, kushusha bendera chakavu na kupandisha mpya, uenezi wa itikadi za ACT-Wazalendo kwa vijana na kufanya shughuli za kijamii.

Mengine ni kufanya makongamano ya kuwaelimisha vijana kuhusu haki zao, kuibua changamoto zao na kuzisemea pamoja na operesheni ya mtaa kwa mtaa jijini Dar es Salaam.

“Leo tunatimiza mwaka mmoja na nusu tangu tuingie madarakani, tuna mpango kazi wa kila mwaka na leo tumeuzindua wa 2022/23. Mbali na kuzindua mpango huo tumejipanga kuendelea kutekeleza mipango kazi mingine,” amesema Kamugisha.

Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Bara, Dorothy Semu, amewataka viongozi wa ngome nyingine kuiga mfano wa vijana Dar es Salaam.

“Ni jambo la kujifunza, wamepewa nafasi ya kuongoza wameweka mikakati yao watafanya nini na nashauri kwa viongozi wengine kuiga mfano mfano kufanya Kazi nzuri ikiwemo kuendelea kusajiki wanachama kidigitali,” amesema Semu.

Naye Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Renatus Pamba, amewataka viongozi wa kitaifa wa Chama hicho, kuwaunga mkono vijana ili watekeleze shughuli zao kuwahamasisha vijana wengine wajiunge.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia kuzindua programu ya nishati safi ya kupikia kwa wanawake Afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua programu ya...

Habari za Siasa

AG aiagiza kamati ya maadili kuwashughulikia mawakili wanaokiuka maadili

Spread the loveMWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Eliezer Feleshi, ameagiza Kamati...

Habari za Siasa

Jaji avunja ukimya sakata la Mpoki kusimamishwa uwakili

Spread the loveJAJI Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amekitaka Chama cha...

Habari za Siasa

Sheikh Ponda ataka mwarobaini changamoto uchaguzi 2020

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa...

error: Content is protected !!