Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Biashara NMB yazindua hati fungani mpya ya trilioni 1
Biashara

NMB yazindua hati fungani mpya ya trilioni 1

Spread the love

BENKI ya NMB imezindua rasmi programu mpya yenye hati fungani zenye thamani ya jumla ya Sh. trilioni moja, huku ikitajwa kuwa ya kwanza kwa ukubwa kusini mwa Jangwa la Sahara. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Akizungumza katika uzinduzi huo leo Jumatatu, Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna amesema kwa kuanzia, programu hiyo ya miaka 10, imeanza leo na toleo la kwanza la hati fungani ya Sh. bilioni 75, itakayodumu kwa miaka mitatu, ikipewa jina la Hati Fungani ya Jamii (NMB Jamii Bond).

Kwa mujibu wa Zaipuna, kiasi hicho kilichoanza jana kinaweza kuongezwa kwa Sh. bilioni 25 zaidi kutegemea na mwelekeo wa soko utakaojitokeza.

Zaipuna amebainisha fedha zitakazokusanywa zitatumika kutoa mikopo inayolenga nishati mbadala na mazingira katika maeneo kama: kuzuia na udhibiti wa uchafuzi mazingira, usimamizi wa majisafi na majitaka na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

“Pia itakuwa ni kwa ajili ya mikopo ya kuwawezesha wanawake na usawa wa kijinsia, nyumba nafuu, usalama wa chakula, huduma za afya, elimu na vijana,” amesema na kuingeza;

“NMB Jamii Bond ina dhamiria kukusanya fedha ambazo zitatuwezesha kutoa mikopo inayolenga kuleta matokeo chanya kwenye jamii kupitia miradi ya mazingira, miradi inayogusa wanawake na vijana, miradi inayolenga kuhakikisha usalama wa chakula, nyumba za bei nafuu, afya, elimu na miradi mingine mingi,” amesema.

Amefafanua kuwa taarifa kuhusu Hati Fungani ya NMB Jamii (NMB Jamii Bond) itawawezesha wawekezaji kupata riba ya asilimia 9.5 kwa mwaka na italipwa mara nne kwa mwaka.

“Kiwango cha chini cha uwekezaji – Sh 500,000. Muda wa uwekezaji – miaka mitatu. Ofa imefunguliwa 25 Septemba 2023 na itafungwa 27 Oktoba 2023,” amesema.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Msajili Wa Hazina – Nehemiah Mchechu, Mwenyekiti wa Bodi ya NMB, Dk. Edwin Mhede; Afisa Mtendaji Mkuu wetu, Ruth Zaipuna; Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) –

CPA. Nicodemus Mkama na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Mary Mniwasa; pamoja na wawakilishi kutoka taasisi za ndani na nje ya nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Cheza sloti ya Zombie Apocalypse na ushinde kirahisi

Spread the love Wengi wetu hupenda filamu za Mazombie huwa zinatishakidogo lakini...

Biashara

Ushirikishwaji wa wafanyakazi ni muhimu katika utekelezaji wa sera za afya na usalama kazini

Spread the love  KILA ifikapo Aprili 28 ya kila mwaka, dunia huadhimisha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Biashara

Wazir Jr kinara wa ufungaji KMC FC ajiunga Meridianbet

Spread the love    MUITE Wazir Jr ‘The King of CCM Kirumba’,...

error: Content is protected !!