Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia apewa tano ujenzi barabara Mtwara
Habari Mchanganyiko

Rais Samia apewa tano ujenzi barabara Mtwara

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

WANANCHI wa Mkoa wa Mtwara, wameishukuru Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara, kitendo kinachoimarisha shughuli zao za kiuchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mtwara…(endelea).

Pongezi hizo zimetolewa hivi karibuni na baadhi ya wananchi wa Mtwara, baada ya Rais Samia kumalizia ziara yake katika mikoa ya kusini.

Dereva wa daladala zinazosafirisha abiria kutoka Soko Kuu hadi Naliendele, Alex Luka amesema baada ya barabara ya Mtwara-Newala-Masasi, kuboreshwa imewasaidia kuondokana na changamoto ya vyombo vyao kuharibika mara kwa mara, pamoja na kuokoa muda.

“Uboreshaji wa hii barabara unatusaidia kupita katika majira yote sababu mwanzoni ilivyokuwa rough road wakati wa masika ilikuwa haipitiki na vyombo vyetu kuharibika. Lakini Sasa hivi imetengenezwa tunaitumia vizuri na tunamshukuru Rais Samia kwa hili,” amesema Luka.

Naye dereva wa bodaboda, Mohamed Mfaume, amesema “tunamshukuru Rais kwa kutuboreshea barabara hii maana miundombinu ya mara ya kwanza ilikuwa mibovu tukawa tunapata shida hususan wakati wa masika barabara haipitiki mvua ikinyesha tunawarushia matope abiria lakini Sasa hivi tunapita vizuri.”

Kwa upande wake Inno Mayunga, amesema baada ya barabara hiyo kurekebishwa, wanaokoa muda wa kusafirisha abiria.

“Ujenzi wa barabara hii ni fursa kwetu madereva wa bodaboda sababu tunatumia muda mfupi kumfikisha abiria anakotaka kwenda tofauti na ilivyokuwa nyuma sababu ilikuwa mbovu. Tunamshukuru Rais Samia kwa hili,” amesema Mayunga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!