RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawaasiliano Tanzania (TTCL), Maharagande Chande, kuwa Postamasta wa Shirika la Posta Tanzania, ikiwa ni siku mbili tangu alivyomuondoa Mkugugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa Leo Jumatatu na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, ikiwa ni siku mbili tangu Rais Samia ateua viongozi 27, tarehe 23 Septemba 2023.
“Rais amemdoa Chande kuwa Postamasta, Shirika la Posta Tanzania, kabla ya uteuzi Chande aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TTCL,” imesema taarifa ya Yunus.
Taarifa ya Yunus imesema kuwa, Chande anachujua nafasi ya Macrice Mbodo, ambaye atapanguwa kazi nyingine.
Baada ya Chande kuhamishwa TTCL, Rais Samia amemteua Mhandisi Peter Ulanga, kuendelea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo.
“Uteuzi huu unaanza mara moja na Balozi mteule Ulanga ataapishwa arehe 26 Septemba 2023, Ikulu jijini Dar es Salaam,” imesema taarifa ya Yunus.
Leave a comment