Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Selasini na wenzake kortini, uamuzi kutolewa leo
Habari za SiasaTangulizi

Selasini na wenzake kortini, uamuzi kutolewa leo

Spread the love

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeanza kusikiliza ombi namba 150 la mwaka 2022 lilifunguliwa na wanachama wawili wa Chama cha NCCR-Mageuzi wakiomba Mahakama hiyo iwazuie Selasin na wenzake tisa kutoratibu au kuitisha Mkutano au kikao chochote cha chama hicho. Anaripoti Juliana Assenga (UDSM) na Faki Sosi…(endelea).

Maombi hayo yamefunguliwa jana tarehe 6 Septemba 2022 na Angelina Mutahiwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara, na Hemedi Kanoni.

Wajibu maombi ni pamoja na Haji Ambar  Khamis, Martha Chiomba, Ameir Mshindani Ali, Susanne Masele, Beati Mpitabakana, Martin Mng’ong’o, Ramadhan Manyeko,  Joseph Selasini, Hassan Ruhwanya, na Bodi ya Wadhamini ya NCCR-Mageuzi (Registered Trustees Of NCCR-Mageuzi.

 

Leo mbele ya Jaji Edwin Kakolaki waombaji kupitia wakili wao Juma Nassor waliwasilisha maombi manne ikiwa ni pamoja na Mahakama itangaze Mkutano wa Halmashauri ulioratibiwa na wadaiwa tarehe 21 Mei 2022 uliofanyika Salvation army ni batili na maamuzi ya mkutano huo yote ni batili.

Ikumbukwe kuwa tarehe 21 Mei 2022 Joseph Selasini na wenzake walitangaza kumsimamisha uenyekiti James Mbatia.

Ombi la pili Mahakama itamke kuwa wadaiwa hawana Mamlaka ya kuitisha vikao vya Kamati Kuu Halmashauri Kuu Vikao vya Sekretieti vya NCCR-Mageuzi.

Tatu Mahakama hiyo ibatilishe vikao vilivyoitishwa tarehe 8,9 10  Septemba 2022.

Nne, amri ya zuio la kudumu dhidi ya mdaiwa wa kwanza mpaka tisa juu uaandaji , uitishaji wa Vikao vya Kamati Kuu, Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi.

Wajibu maombi  waliohudhuria mahakamani hapo ni pamoja na mjibu maombi namba tano Mpitabakana na Mng’ong’o mjibu maombi namba sita huku Mohammed Tibanyendela na Thomas Nguma wakiiwakilisha bodi ya wadhamini ya chama hicho.

Wakati huo huo Wakili Nassoro aliiomba Mahakama hiyo kutoa zuio la vikao vyote ndani ya chama hicho.

“Maombi yameombwa chini ya hati ya dharura, kuna vikao vinaendelea leo, kesho, tarehe 8 na tarehe 15 ambavyo vitaathiri shauri hili tumeomba ziuo kwa wajibu maombi kutoenndelea na vikao hivyo mpaka maombi hayo yatakaposikilizwa na kuamriwa,” amesema Nassoro.

Mjibu maombi namba tano Mpitabakana aliulizwa na mahakama endapo anakubaliana na ombi la waombaji la kutaka kuzuiwa kwa mikutano, akaeleza kuwa hakubaliani nalo kwa kuwa shughuli za chama cha siasa zikizuiwa maendeleo ya chama yatadorora.

“Chama ni vikao kama kutakuwa hakuna vikao kitakuwa mfu huwezi kuamua jambo kama wewe Katibu Mkuu pekee yako lazima uite vikao,” amesema Mpitabakana.

Naye Mng’ong’o mjibu maombi namba sita aliomba muda wa kujibu kikoa .

Alipoulizwa kuhusu kuzuiwa vikao alijibu “Mimi kiongozi sijapokea wito wa kikao kwa tarehe hizo …wangesema wataathirika vipi wawasilishe ajenda ambayo wanaona wao kuwa itawaathiri ili isijadiliwe mpaka uamuzi,” ameeleza.

Aliyewakilisha bodi ya wadhamini aliieleza mahakama kuwa wao kama bodi ya wadhamani walipata nyaraka za maombi hayo jana hivyo wanaomba muda wa kujibu maombi hayo.

“Mleta maombi namba moja namtambua ni Makamu Mwenyekiti Bara, hivyo vikao vinavyoombwa vizuiliwe ndivyo vilivyoleta mtafaruku ndani ya chama kuna vikao kadhaa ndivyo vilivyoleta mgogoro hivyo vikizuiwa havitakuwa na athari ndani ya chama tutajibu mapema ili shughuli za chama ziendelee,” amesema.

Wakili Nassoro akijibu hoja za wajibu maombi namba tano na sita alieleza mahakamani hapo kuwa ameomba wajibu maombi wasishiriki kwenye vikao vya chama.

“Nimeomba wajibu maombi namba moja mpaka tisa kuzuiwa kushiriki na kuitisha vikao, hakuna aliyetoa sababu za kwanini zikao hivyo visizuiliwe. Nimeomba hawa mjibu maombi namba moja mpaka wa tisa wasishiriki kwenye vikao lakini vikao muhimu kwenye  chama viendelee”

Jaji Kakokolaki ameahirisha shauri hilo ambapo amesema anapitia hoja zote na kwamba saa tisa alasiri atatoa uamuzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!