RAIS Samia Suluhu Hassan amempongeza Liz Truss kwa kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Uingereza na kuchukua nafasi ya Boris Johnson. Anaripoti Apaikunda Mosha, TUDARCo … (endelea).
Rais Samia ametoa pongezi hizo leo tarehe 7 Septemba, 2022 kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kuandika hivi; “Hongera kwako @trussliz kuwa kuchaguliwa kuwa Kiongozi mpya wa chama cha Conservative na Waziri Mkuu wa Uingereza. Tanzania inatarajia kuendeleza urafiki wake wa muda mrefu na Uingereza katika kukuza uhusiano wetu wa kiuchumi na kidiplomasia.”
Truss amechukua nafasi ya Johnson aliyewasilisha rasmi barua ya kujiuzulu kwake kwa Malkia Elizabeth II katika eneo lake la Balmoral huko Scotland na malkia kumteua Truss kuwa waziri mkuu.
Truss mwenye umri wa miaka 47 anakuwa mwanamke wa tatu kuongoza nchi hiyo na waziri mkuu wa nne wa Uingereza katika kipindi cha miaka sita.
Truss alishinda katika kura ya ndani ya chama Jumatatu wiki hii na kumshinda Waziri wa zamani wa Fedha, Rishi Sunak.
Baada ya ushindi wake kutangazwa, Truss aliuambia mkutano wa chama hicho; “Nilifanya kampeni kama M-Conservative na nitawaongoza kama M-conservative”.
Leave a comment