Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Ruto azungumza na Rais Kenyatta
KimataifaTangulizi

Ruto azungumza na Rais Kenyatta

Spread the love

HATIMAYE Rais mteule wa Kenya, Dk. William Ruto leo Jumatano amezungumza na Rais Uhuru Kenyatta wa taifa hilo anayemaliza muda wake madarani. Wawili hao wamzungumza kwa njia ya simu ikiwa ni zaidi ya miezi miwili tangu wawili hao wazungumze.

Ruto ambaye pia ni Naibu Rais, kupitia ukurasa wake wa Twitter, leo tarehe 7 Septemba, 2022 amethibitisha kuzungumza ka Rais Kenyatta. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

“Nimefanya mazungumzo ya simu na bosi wangu, Rais Uhuru Kenyatta. Tumejadili Uchaguzi Mkuu uliomalizika hivi karibuni na mchakato wa kipindi cha mpito kama ilivyo mila na desturi zetu za demokrasia” ameandika Ruto.

Hatua hiyo imetajwa kuwa mwanga mzuri kuelekea mchakato wa kuapishwa kwa Rais huyo mteule siku ya Jumanne tarehe 13 Septemba, mwaka huu.

Itakumbukwa kuwa juzi Jumatatu muda mfupi baada ya Mahakama ya Juu nchini Kenya kutupilia mbali maombi ya kikatiba yayolifunguliwa wiki iliyopita na mgombea aliyeshindwa, Raila Odinga kupinga ushindi wa Ruto, Ruto alibainisha kuwa wawili hao hawajazungumza kwa zaidi ya miezi huku akiahidi kuwa atampigia simu kuzungumza naye.

“Nina miezi sasa sijazungumza naye lakini nitampigia rafiki yangu Rais Uhuru Kenyatta tuzungumze” alisema Ruto.

Aidha, siku hiyo baadaye Rais Kenyatta akilihutubia taifa alisema kuwa mchakato wa makabidhiano ya madaraka kwa utawala mpya unaendelea huku akisisitiza kuwa yatakuwa ya amani.

Rais Kenyatta alisema anaheshimu uamuzi wa Mahakama ya Juu wa kuidhinisha ushindi wa Ruto kama Rais mteule.

“Nilipoapishwa kuwa Rais, niliahidi kuheshimu sheria. Leo Jumatatu Mahakama ya Juuu imeidhinisha matokeo ya urais kama yalivyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC). Ninaheshimu uamuzi wa Mahakama” alisema Kenyatta ambaye katika kipindi cha kampeni za uchaguzi huo uliofanyika tarehe 9 Agosti mwaka huu alikuwa anamuunga mkono Odinga,

Katika hotuba yake, Rais Kenyatta hakumtaja kwa jina Rais mteule William Ruto wala kumpongeza kwa ushindi wake lakini aliwapongeza Wakenya kwa kudumisha amani wakati wote wa mchakato wa uchaguzi na wakati matokeo yalipopingwa mahakamani hali iliyozidisha maswali miongoni mwa raia wa Kenya kuhusu hatima ya wawili hao.

Katika matokeo ya uchaguzi wa Rais yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Wafula Chebukati tarehe 15 Agosti, 2022, Ruto alishinda kwa kura 7,176,142 (asilimia 50.49 ya kura) na Odinga akafuatia kwa kura 6, 942, 930 (asilimia 48.85).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

error: Content is protected !!