Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Bei ya petroli, dizeli yashuka
Habari MchanganyikoTangulizi

Bei ya petroli, dizeli yashuka

Spread the love

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei ya kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli ambapo zimeshuka hadi Sh. 2,969 kwa petroli na dizeli Sh 3,125 kwa mkoa wa Dar es Salaam. Anaripoti Felister Mwaipeta, TUDARCo … (endelea). 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na EWURA bei hizo zimepungua baada ya bei ya mafuta katika soko la dunia za Julai kupungua ikilinganishwa na bei za Juni, 2022.

Bei hizo ambazo pia zimewekewa ruzuku ya Serikali zitaanza kutumika kuanzia kesho tarehe 7 Septemba, 2022.

Bei ya petroli kwa mkoa wa Tanga na Mtwara ni Sh 3,033 na Sh 3,082 huku dizeli ikiwa ni Sh 3,131 na Sh 3,213 matawalia.

Kwa upande wa mafuta ya taa ambayo hayajawekewa ruzuku bei ni Sh 3,335 kwa mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.
Bei hizo ni za chini ikilinganishwa na zile za mwezi Agosti ambapo petroli iliuzwa kwa Sh 3410 huku dizeli ikiwa Sh 3322 kwa mkoa wa Dar es Salaam.

Kwa mikoa ya Tanga na Mtwara bei ya mwezi Agosti petroli ilikuwa Sh 3435 na 3393 huku dizeli ikiwa Sh 3349 na Sh 3351 mtawalia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari Mchanganyiko

GGML yasisitiza kuendelea kuimarisha afya za wafanyakazi

Spread the loveKAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited kwa kushirikiana na kampuni...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!