RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake inafanyia kazi changamoto ya upungufu wa walimu nchini, huku akiweka wazi mpango wake wa kutaka kuwajengea nyumba walioko kazini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Mkuu huyo wa nchi akizungumzia ziarani mkoani Singida, leo tarehe 16 Oktoba 2023, amesema kwa sasa nchi inakabiliwa na upungufu wa asilimia 40 ya walimu wa shule ya msingi na asilimia 26 wa shule za sekondari.
“Suala hili tunakwenda kulifanyia kazi na nimearifiwa kuwepo uhitaji wa nyumba za walimu, hili tunalijua nataka niwahakikishie bajeti ya mwakani Serikali itajielekeza zaidi kwenye ujenzi wa nyumba za walimu. Tumeanza kujenga lakini ni kweli hazijatosha na walimu wanashindwa kukaa maeneo yao kutokana na upungufu wa nyumba,” amesema Rais Samia.
Akizungumzia maendeleo ya sekta ya elimu, Rais Samia amesema serikali yake inaendelea kupeleka fedha katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi pamoja na uendeshaji wa sera ya elimu bila malipo.
Leave a comment