RAIS Samia Suluhu Hassan amesema shughuli za kuleta maendeleo katika nchi ni hatua na kuwahakikishia wale ambao bado hawajafikiwa na huduma mbalimbali kuwa zitawafikia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma … (endelea).
Mkuu huyo wa nchi amesema maendeleo hayawezi kuja ndani yam waka mmoja au miwili na kuweza kuridhisha watu wote.
Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu tarehe 17 Oktoba, 2022, akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa barabara ya Kasulu na uwekaji jiwe la msingi wa barabara ya Kasulu Manyovu mkoani Kigoma.
Amesisitiza kuwa maendeleo ni safari, “tumeanza na tunakwenda waliopata maji wamshukuru ambao bado tunawahakikishia watapata, waliopata umeme wafurahie waendelee kufanya kazi, ambao bado umeme uko njiani unakuja, waliopata barabara wafurahie ambao bado barabara zinakuja.”
“Kwahiyo ni hatua kitu kikubwa kwetu ni kuwahakikishia tumetumwa na Chama Cha Mapinduzi kutekeleza ilani yao na tutaitekeleza jinsi mungu atakavyotujalia jinsi uchumi utakavyoruhusu,” amesema.
Ameeleza kuwa ili Seriklai iweze kutekeleza ni lazima wananchi wachape kazi kwa bidii ili kila mtu awe na mchango kwenye maendeleo ya taifa.
Akizungumzia suala la uhaba wa mbolea katika mkoa huo amesema mahitaji yameongezeka baada ya kuanza kwa utaratibu wa ruzuku na kuwahakikishia kuwa tatizo hilo litatatuliwa ndani ya wiki moja hadi mbili.
“Mawakala Kigoma ni wachache tupeni wiki moja, mbili tunakwenda kuongeza mawakala Kasulu na Kigoma mawaziri watakuwa hapa kuhakiisha mbolea inatoka. Mnafaya vizuri kwenye kujiandikisha lakini kwenye namba mtandao unasumbua kidogo lakini nimeongea na Waziri amenihakikishia wataongeza mawakala na kurekebishaa tatizo la upatikanaji wa namba.”
Leave a comment