Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia awaita wawekezaji, ‘sekta hii ina faifa kubwa”
Habari za Siasa

Samia awaita wawekezaji, ‘sekta hii ina faifa kubwa”

Spread the love

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewaita wawekezaji wa sekta binafsi kuja kushirikiana na serikali katika sekta ya uchimbaji gesi asilia. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumamosi, Ikulu jijini Dodoma, wakati akishuhudia hafla ya utiaji saini mikataba ya mauziano na uendeshaji wa kitalu cha gesi cha Mnazi Bay mkoani Mtwara, kati ya TPDC na Kampuni ya Maurel & PROM kutoka nchini Indonesia.

“Pamoja na kwamba sekta hii inayo faida lakini kwanza lazima jasho likutoke halafu ndio uone faida, sasa kutokana na miradi hii kuwa na gharama kubwa hekima inatuongoza kuwa shughuli hizi zifanywe kwa ubia na wenzetu wa sekta binafsi ambao kwao inatoka mitaji, ujuzi, ubobebzi na teknolojia ya kisasa. Sisi kwetu hatuna ndio maana tunakaribisha sekta binafsi tufanye nayo kwa karibu,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema tayari Tanzania imeanza kuonja mafanikio ya utajiri kwa gesi kwa kuwa inachangia asilimia 65 hadi 70 ya uzalishaji umeme, wakati viwanda 56 vikunganishwa na nishati hiyo.

Akizungumzia mradi huo, Makamu wa Rais Dk. Phillip Mpango amesema ni vyema watanzania washirikishwe katika uvunaji wa gesi hiyo, huku akisema mradi ukianza uatsaidia kuongeza upatikanaji umeme pamoja na kusaidia matumizi mengine yanayotumia gesi kama vile magari.

“Naomba niseme moja tu, maendeleo ya nchi yoyote yanategemea namna ambavyo taifa hilo linatumia rasilimali zake na Tanzania imejaaliwa rasilimali nyingi na mojawapo ni rasilimali ya gesi asili. Sasa ili uweze kuitumia yako mambo ya msingi ambayo ni lazima yazingatiwe.

“Moja ni umiliki wa rasilimali yenyewe, unaweza kuwa na rasilimali usiimiliki na hivyo haitawasaidia watu wako, la pili ni muhimu sana watu wako washiriki katika uvunaji wa ile rasilimali na maendeleo yake,” amesema Dk. Mpango.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mussa Makame (kulia) pamoja na Meneja Mkazi wa M &P Exploration Production Tanzania Limited Nicolas Engel (kushoto) wakionesha Hati ya Mkataba wa Mauziano ya Hisa katika Kitalu cha uzalishaji wa Gesi Asilia cha Mnazi bay baina ya (TPDC) na Kampuni ya M&P kwenye hafla iliyofanyika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 3 Februari 2024.

Naye Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemshukuru Rais Samia kwa kuridhia mradi huo wa uchimbaji visima vya gesi, uwekaji wa mitambo ya kusukuma kujengwa Mtwara akisema itasaidia na mikoa jirani hususan Lindi.

“Nataka nikuhakikishie na wabunge wenzangu wa Mtwara na Lindi hatutakuangusha kwa maendeleo uliyoyaleta Lindi. Lindi na Mtwara wako hapa mimi miongoni mwao wa wanufaika wa miradi huo,” amesema Waziri Majaliwa.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Dotto Biteko, amesema mikataba hiyo ni matokeo ya kazi kubwa iliyofanywa na timu ya wataalamu iliyoundwa kwa ajili ya kufanya majadiliano na wawekezaji, ambapo walitanguliza mbele maslahi ya Tanzania licha ya mashinikizo waliyokutana nayo.

Amesema hafla hiyo ni utekelezaji wa maagizo yake ya kutaka utekelezaji wa haraka wa makubaliano aliyofanya na Rais wa Indonesia, Joko Widodo.

Aidha, Dk. Biteko amesema wizara yake imeanza kufanyia kazi utekelezaji wa agizo lake la kuhakikisha maisha ya wananchi wanaoishi maeneo yanayokochimbwa gesi yanabadilika na kuwa mazuri kwa kufikisha huduma muhimu hasa vituo vya afya, barabara na umeme.

“Ziara unazofanya kwenye mataifa mbalimbali ni kielelezo kwamba yale unayokubaliana sisi kwetu sio kuweka kwenye makabati ni working tools kufanya hivi vitu vitokee. Na ulivyoniambia mahali ambako gesi inachimbwa mfanye utaratibu maisha ya watu yabadilike , nakubali na lazima tuchukue hatua,” amesema Dk. Biteko.

3 Comments

  • Je, gesi itasambazwa nchini au tutawauzia Kenya?
    Ni lini kukatandika mabomba ya gesi nchini na kutumia wataalamu wetu wenyewe.
    Tungepeleka wanafunzi urusi, ambao ni mabingwa wa gesi tungeshakuwa na gesi nchi nzima.

  • Maurel and prom siyo kampuni ya Indonesia. Ni kampuni ya Ufaransa ambayo in tawi huko, Venezuela, Gabon, Namibia na kwingineko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!