Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge CCM wafunguka miswada uchaguzi kupitishwa bungeni
Habari za Siasa

Wabunge CCM wafunguka miswada uchaguzi kupitishwa bungeni

Dk. Pauline Nahato
Spread the love

BAADHI ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamesema hatua ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kukubali marekebisho ya sheria za uchaguzi imeonesha dhamira yake ya kutafuta maridhiano na kuijenga upya Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Maoni hayo yalitolewa jana Ijumaa, baada ya muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa 2023; Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi wa 2023 na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa 2023, kupitishwa bungeni jijini Dodoma kwa ajili ya kuwa sheria baada ya kusainiwa na Rais Samia.

Mbunge viti maalum, Dk. Pauline Nahato alisema miswada hiyo imebeba maoni ya wadau juu ya maboresho ya mifumo ya uchaguzi, hasa kifungu kinachopendekeza mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kupendekezwa badala ya kuteuliwa moja kwa moja na Rais.

“Siku ya leo (jana) imekuwa ya kipekee sana katika Bunge letu kwa sababu imekuwa ni siku ambayo tumeijadili na kuridhia miswada iliyoletwa bungeni ambayo imepitia michakato muhimu sana.

Maimuna Pathan

“Napenda kumshukuru Rais Samia kwa kuridhia miswada kuja bungeni na kujadiliwa kwa uwazi kabisa. Kabla ya kuja bungeni imejadiliwa na watu wa makundi mbalimbali, wanasiasa, viongozi wa dini na wa vyama vyote,” amesema Dk. Nahato.

Naye Mbunge Viti Maalum mkoani Lindi, Maimuna Pathan, alisema miswada hiyo imebaba maoni yote yaliyotolewa na wadau na kwamba hakuna pendekezo lililoachwa.

“Mama yetu, Rais wetu Dk. Samia amefanya kitu ambacho anastahili sana apewe maua yake. Ni kitu kikubwa anatakiwa apongezwe ameonyesha mshikamano na ushirikiano, amekubali kupokea maoni yaliyotoka kwa wadau wote nje kwa wapinzani na waliomo ndani ya chama na watu mbalimbali. Amefanyia kazi bila kuyabagua ameyaleta bungeni yamejadiliwa kwa uwazi na kupitishwa,” amesema Maimuna.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!