Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Chadema kuwasilisha muswada binafsi bungeni kudai katiba mpya
Habari za Siasa

Mbunge Chadema kuwasilisha muswada binafsi bungeni kudai katiba mpya

Aida Khenani
Spread the love

MBUNGE wa Nkasi Kaskazini (Chadema), Aida Khenani, amesema anakusudia kuwasilisha bungeni muswada binafsi wa kudai ufufuaji mchakato wa upatikanaji katiba mpya.

Khenani amenuia kuchukua hatua hiyo baada ya kudai kuwa Serikali imepuuza maoni ya wadau kuhusu suala hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Khenani ametoa kauli hiyo jana Ijumaa, bungeni jijini Dodoma, baada ya kugoma kushiriki majadiliano na upitishaji miswada ya marekebisho ya sheria za uchaguzi.

Mbunge huyo wa Chadema alidai kuwa, mapendekezo mengi ya wadau kuhusu marekebisho ya katiba hayajaingizwa katika miswada hiyo, ndio maana aliamua kutoka nje ya Bunge wakati vifungu vyake vikijadiliwa.

“Nimetoka bungeni sababu nimeona hakuna haja ya mimi kuwepo kwa sababu nilitegemea kama ratiba ilivyokuwa inaonyesha kwamba tungejadili mpaka leo (jana Ijumaa), lakini Spika Tulia Ackson amesema kulingana na ukubwa wa miswada mitatu lazima siku ya leo itumike kwa serikali kujibu. Hivyo leo hakuna aliyechangia ndio maana sijaona haja ya kuendelea kuwepo,” alisema Aida na kuongeza:

“Pia msimamo wa chama changu ni miswada hiyo kuondolewa bungeni kabla haijapitishwa sababu maoni ya wadau hayajaingizwa mule, mimi kama mbunge nina haki nyingine, nakusudia kuleta muswada binafsi kwa ajili ya kukwamua ile katiba mpya, mchakato uanze upya tufanye marakebisho ya katiba.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!