Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia ashiriki mkutano wakuu wa nchi EAC
Habari za Siasa

Samia ashiriki mkutano wakuu wa nchi EAC

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan leo Ijumaa ameungana na viongozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC, kufanya mkutano wao wa kawaida nchini Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kwa sasa, EAC inajumuisha nchi saba: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Uganda na Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit kabla ya kuanza kwa Mkutano wa ndani wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Ngurdoto Mkoani Arusha tarehe 24 Novemba 2023

Ajenda ya mkutano huo wa marais ni pamoja na kupokea ripoti ya majadiliano ya kuidhinishwa kwa shirikisho la Somalia katika EAC.

Mazungumzo ya Somalia kujiunga na EAC yalianza mwezi Agosti mwaka huu, huku kamati maalumu ya nchi za Afrika Mashariki ikifanya mazungumzo na Somalia kuhusu ombi lao.

Marais pia watajadiliana kuhusu maendeleo ya mchakato wa Nairobi unaoongozwa na EAC kuhusu kurejesha amani Mashariki mwa DRC.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud kabla ya kuanza kwa Mkutano wa ndani wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Ngurdoto Mkoani Arusha tarehe 24 Novemba 2023

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ilituma wanajeshi kwa mara ya kwanza katika eneo hilo lenye hali tete nchini DRC mwezi Novemba mwaka uliopita baada ya kuibuka tena kwa kundi la waasi la M23.

Maeneo haya ya kaskazini mwa DRC ni maeneo yaliyoshuhudia mashambulizi kutoka kwa vikundi vyenye silaha, yanaendelea kutishia juhudi za amani na utulivu zilizopatikana hadi sasa.

Hata hivyo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanasema vikosi vya Kanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACRF) vitaondoka nchini humo kufikia tarehe 8 Disemba.

DRC imekataa kikosi hicho kuongeza muda zaidi ikidai wanajeshi wa Afrika Mashariki hawajaweza kutatua tatizo la ukosefu wa usalama hasa lile la mashambulizi kutoka kwa waasi wa M23.

DRC inasema ingependelea nchi za Afrika Kusini kutuma majeshi huko.

Rais wa Kenya, Dk. William Ruto akishiriki Mkutano wa Ndani wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Ngurdoto Mkoani Arusha tarehe 24 Novemba 2023

Mwezi Novemba marais wa Jumuiya ya nchi za Kusini mwa Afrika, SADC, walikutana mjini Luanda nchini Angola, kuzungumzia hali ya usalama Mashariki mwa DRC.

Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kukamilisha mpango wa kupeleka vikosi vya kijeshi hivi karibuni nchini DRC (SAMIDRC).

Marais katika mkutano wao pia watajadili maendeleo ya mbinu endelevu za ufadhili wa EAC na kufanya mashauriano ya katiba ya shirikisho la kisiasa la EAC.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir anatarajiwa kushika uenyekiti wa Jumuiya ya EAC kutoka kwa mwenzake wa Burundi rais Evariste Ndayishimiye ambaye muda wake wa uenyekiti umefikia ukomo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!