Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sakata la DP World na bandari lafufuka upya
Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the love

SAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati ya Dubai, juu ya ushirikiano wa uwekezaji kwenye baadhi ya maeneo ya Bandari ya Dar es Salaam, halijakwisha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Ni baada ya Wakili Boniface Mwabukusi, kueleza kwamba wametinga katika Mahakama ya Rufaa Kanda ya Mbeya, kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu, Kanda ya mkoa huo, kutupilia mbali kesi waliyofungua kuzuia utekelezaji wa mkataba huo kwa madai kuwa hauna maslahi kwa taifa.

Wakili Mwabukusi

Mwabukusi ametoa msimamo huo leo tarehe 20 Februari 2024, katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), uliofanyika jijini Mbeya.

“Mungu anapoumba eneo au taifa lolote anakupa ardhi, mipaka yako, anga lako na rasilimali asili ambayo zinakuwa mambo hayawezi kugawanyika au kuwekwa chini ya mikono ya wageni. Serikali ya CCM inakabidhi rasilimali zote za asili kwa mikataba ya kizembe kupitia mwakilishi kutoka hapa Mbeya, ndiye anayekaa katika Bunge kuongoza kama spika,” amesema Mwabukusi na kuongeza

“Katika hali ya ajabu sisi tumeenda mahakamani, saa hizi kesi inaenda mahakama ya rufaa kuna watu wanasema suala la bandari limekwisha, tumewaambia hivi tulishatamka na tunarudia bandari ni urithi wetu haitauzwa kambwe na wala haitakwenda kwenye mikono ya wageni.”

Sakata hilo lilitulia kidogo, baada ya Serikali na Kampuni ya DP World ya Dubai, kusaini mikataba ya kuanza uwekezaji bandarini, ambapo mara kadhaa imekuwa kuna taratibu za kisheria zinakamilishwa ili ianze kazi.

Serikali imekuwa ikitoa ufafanuzi juu ya madai ya watu wanaopinga uwekezaji huo, ikisema mkataba wake unalinda maslahi ya nchi na kwamba DP World itafuatiliwa kwa karibu katika utendaji kazi wake na ikibainika inakwenda kinyume mkataba unaweza kuvunjika.

3 Comments

  • Mikataba yote ina mwanzo na mwisho. Miaka ni mitano ili kulinda uwajibikaji. Huhitaji kuwa mwanasayansi wa roketi kujua mkataba mzuri na mbovu.

  • Unaposema Kuna miaka 5 ya kuchunguza kama DP World anatekeleza ipasavyo masharti ya mkataba vinginevyo utavunjwa.
    Swali la msingi hapa ni je vipengele vya uvunjaji wa mkataba viko rafiki kuruhusu hilo kufanyika?

  • Mnaposena kuna miaka 5 ya kuchunguza utetelezaji wa mkataba na kama DP World asipotekeleza ipasavyo masharti mkataba utavunjwa. Swali la msingi ni je vipengele vya uvunjaji wa mkataba viko rafikiki kiasi gani kwa hilo kutendeka?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!