Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa SAKATA LA CORONA: Mipaka kufungwa Ulaya
KimataifaTangulizi

SAKATA LA CORONA: Mipaka kufungwa Ulaya

Spread the love

KUIBUKA upya kwa ugonjwa wa Corona ulimwenguni, kunaweza kusababisha mataifa kadhaa ya Ulaya, kufunga mipaka yake, ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo. Anaripoti Saed Kubenea, Dar es Salaam … (endelea).

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amenukuliwa jana Jumatano akisema, taifa hilo, laweza kufunga mipaka yake, iwapo majirani zake hawatadhibiti kikamilifu kusambaa kwa virusi vipya vya Corona.

Amesema, Ujerumani ambayo iko chini ya vizuizi vya kufunga shughuli zake, itahitaji kufunga mipaka yake, ikiwa mataifa mengine yatashindwa kuchukua hatua za dharura kuzuia kusambaa zaidi kwa ugonjwa huo. 

Huku Ujerumani ikitishia kufunga mipaka yake, viongozi wa Umoja wa Ulaya (EU), wamepanga kukutana leo Alhamisi, kujadili ongezeko la virusi vipya vya Corona.

Katika mkutano huo, ambao unafanyika kwa njia ya video, viongozi wa Ulaya, wanatarajiwa kujadili kuanzia udhibiti wa usambaaji wa virusi vinavyobadilika hadi kitisho cha kufunga mipaka.

Aidha, viongozi hao watajadili kasi ndogo ya utoaji wa chanjo. Huu utakuwa mkutano wa tisa tangu kuanza kwa janga hilo.

Kamisheni ya Umoja wa Ulaya imesema Jumanne hii kwamba mataifa 27 ya umoja huo yatatakiwa kuwa yametoa chanjo kwa angalau asilimia 70 ya watu wazima hadi ifikapo majira ya joto.

Mataifa ya Ulaya yameelezea wasiwasi, baada ya wiki iliyopita kugundua kwamba chanjo ya Pfizer inayozalishwa na mmoja kati ya wazalishaji wawili waliothibitishwa na EU, huenda ikapunguza kiwango cha usambazaji.

Italia inaangazia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya hatua hiyo ya Pfizer.

Wakati hayo yakiendelea Ulaya, rais mpya wa Marekani, Joe Biden, amesaini amri 17 za rais katika siku yake ya kwanza madarakani, ikiwamo amri ya kupambana na janga hilo nchini mwake.

Mpaka sasa, Corona imewaua watu takribani 405,000 na zaidi ya watu milioni 24 wakiwa wameambukizwa. Kwenye amri hiyo amewataka watu kuvaa kwa lazima barakoa.

Nako nchini China, katika jiji la Shanghai, mamlaka zimeanza kuwahamisha wakaazi wa maeneo jirani baada ya maafisa nchini humo kugundua angalau visa vitatu vya virus vipya vya corona hii leo.

Maafisa hao hata hivyo hawakusema ni watu wangapi hasa wameondolewa kwenye maeneo hayo, katikati ya jiji la Shanghai wakati wakiimarisha zaidi upimaji kufuatia mripuko huo.

1 Comment

  • Ulimwengu umekumbwa na Corona lakini sisi tunafumbia macho’. Hata kama hapa kwetu hakuna maambukizi je vipi wageni wanaoingia kwa vingi na vipi wananchi wetu wanaosafiri nje na kurudi nyumbani? Hawa hawawezi kuja na virusi? Corona haina mipaka. Tusidharau kupima na chanjo kana kwamba tunaishi peke yetu duniani TAFADHALI WATAALAMU SEMENI TUMIENI WELEDI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

Habari za SiasaTangulizi

Haya hapa majina walioteuliwa kugombea nafasi mbalimbali CHADEMA

Spread the loveCHAGUZI wa kanda za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Uingereza yamwaga bil. 9 kumuunga mkono Samia matumizi nishati

Spread the loveWaziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani...

error: Content is protected !!