Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif: Maendeleo makubwa yanahitaji muda
Habari za SiasaTangulizi

Maalim Seif: Maendeleo makubwa yanahitaji muda

Maalim Seif Sharrif Hamad, Aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Spread the love

MAKAMO wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesihi Wazanzibari kuendelea kustahamili shida kabla ya kutarajia matokeo ya haraka ya serikali mpya inayoendeshwa kwa ushirikiano wa vyama viwili kikiwemo cha ACT Wazalendo. Anaripoti Jabir Idrissa, Zanzibar…(endelea).

“Tumeambiwa hapa kwamba serikali hii ambayo na sisi (ACT Wazalendo) ni sehemu, ndio kwanza ina siku 42 tangu ifanye kazi. Ni muda mfupi sana kutarajia mabadiliko makubwa ya kila eneo.

“Ni muhimu mfanye subira zaidi kwa sababu mnajua mambo yalivyokuwa; sasa kazi ya kuyarekebisha ni nzito inayohitaji muda kidogo,” amesema.

Maalim Seif ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa ACT Wazalendo alisema hayo jana Jumatano wakati akijibu hoja na maoni ya wanachama katika mfululizo wa ziara yake kwenye mikoa ya Unguja.

Katika ziara iliyoanza kisiwani Pemba, mwezi uliopita, Maalim Seif alikutana na viongozi wa ngazi zote katika mikoa ya kichama ya Magharibi A na Magharibi B, kwenye ukumbi wa Majid, eneo la Kiembesamaki mjini Zanzibar.

Alisema yeye pamoja na makamo mwenzake – makamo wa pili – wanaendelea kumuunga mkono Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, katika mfumo mpya wa utendajikazi unaohimiza uwajibikaji wa kiwango cha juu na msisitizo wa kuwapa wananchi haki haraka pale wanapozihitajia.

Maalim Seif alisisitiza serikali haitamuonea mtu lakini haina muhali hata chembe kwa yeyote yule anayekwamisha haki za watu kwa sababu binafsi; pamoja na watumishi wanaodai rushwa ndipo wahudumie watu.

Akijibu hoja ya kutaka masheikh waliokamatwa Zanzibar na kupelekwa kushitakiwa kwenye mahakama ya Tanzania na ambao kesi yao inasuasua ikiwa imetimia miaka tisa sasa, alisema anavyojua “suala hili linashughulikiwa.”

Maalim Seif ametaka viongozi wa ACT Wazalendo kuongeza kasi ya kukiimarisha chama hicho ikiwemo kukijengea uwezo wa kushika dola utakapofanyika uchaguzi mkuu.

Dk. Hussein Mwinyi, mwanachama wa CCM aliyetangazwa mshindi wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana, anaongoza serikali ya umoja wa kitaifa aliyoiunda kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 iliyofanyiwa mabadiliko makubwa mwaka 2010 yaliyowezesha kuwepo kwa serikali ya mfumo wa umoja wa kitaifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!