May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mkude ‘achutama’ aomba kusamehewa

Jonas Mkude

Spread the love

KIUNGO wa timu ya Simba na Taifa ya Tanzania, Jonas Mkude ameomba radhi kwa viongozi, wanachama pamoja na mashabiki wa klabu hiyo mara baada ya kufungiwa kwake kutokana na matatizo ya utovu wa nidhamu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)

Mchezaji huyo alifungiwa na uongozi wa Simba tarehe 28 Desemba 2020, kutokana na matatizo ya utovu wa nidhamu ambayo ilimlazimu kukaa nje ya uwanja kwa wiki tatu.

Mkude amomba msamaha huo kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram huku akiahidi kuwa hatokosera tena kwa kuwa timu hiyo ni sehemu ya maisha yake.

“Tumeumbwa kukosea lakini haimanishi nitakosea tena, mimi ni mwanasimba mwenzenu na klabu hii ni sehemu ya maisha yangu, naamini wachezaji wenzangu, benchi la ufundi, viongozi, wanachama na mashabiki mtanielewa na mtanisamehe.” 

Pamoja na Mkude kuomba radhi viongozi, wachezaji na mashabiki wa timu hiyo, lakini kiungo huyo hajaeleza kosa alilofanya, pia klabu ya Simba nao hawakuweza wazi makosa ya nyota huyo.

Ikumbukwe taarifa wakati wa kumfungia mchezaji huyo ilieleza kuwa Mkude atafikishwa kwenye kamati ya nidhamu ya klabu hiyo ili ya shauli lake lisikilizwe.

Toka kufungiwa kwa mchezaji huyo amekosa jumla ya michezo minne ambayo miwili kati ya hiyo ilikuwa ya Ligi Mabingwa Afrika huku mmoja ukiwa wa Ligi Kuu dhidi ya Ihefu na mwengine dhidi ya Maji Maji kwenye michuano ya kombe la Shirikisho.

Mkude ambaye pengine kufungiwa kwake na uongozi wa klabu yake umesababisha kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Ettiene Ndayilagije kutomjumuisha kwenye kikosi kilichoenda Cameroon kwenye michuano ya kombe la mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani.

error: Content is protected !!