Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Rukuba wajenga kituo cha afya, waomba watumishi
Afya

Rukuba wajenga kituo cha afya, waomba watumishi

Spread the love

WAKAZI wa Kisiwa cha Rukuba, Wilaya ya Musoma, mkoani Mara, wameiomba Wizara ya Afya na Wizara Ofisi ya Rais-TAMISEMI, ipeleke watumishi pamoja na vifaa tiba, katika Kituo cha Afya walichokijenga kwa kushirikiana na Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara… (endelea).

Ombi hilo la wananchi limewasilishwa na Ofisi ya Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, leo tarehe 8 Julai 2023.

“Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba wanaiomba Serikali iwapelekee wafanyakazi na vifaa tiba ili Kituo hicho kianze kutoa hudumia kisiwanj hapo. Wakazi wanataka wapunguze kusafirisha wagonjwa mahututi na mama wajawazito kwenye mitumbwi kwenda Musoma Mjini kwa matibabu,” imesema taarifa hiyo.

Aidha, wananchi wa kisiwa hicho wameishukuru Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha kiasi cha Sh. 500 milioni kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kituo hicho ulioanzwa na wananchi kwa kushirikiana na Prof. Muhongo.

Ujenzi wa kituo hicho cha Afya Rukuba, umekamilika na kina majengo manne la mama na mtoto, maabara, upasuaji na ufuaji. Ujenzi huo umetokana na wananchi kupanua iliyokuwa zahanati yao.

Mbali na ukamilishaji wa kituo cha afya cha kisiwa hicho chenye vijiji vinne, Prof. Muhongo kwa kushirikiana na wananchi, wameanza ujenzi wa shule ya Sekondari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

error: Content is protected !!