HALMASHAURI ya mji Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe imetumia kiasi cha Sh 1.7 bilioni kujenga mradi huo wa maegesho ya malori ili kukabiliana na msongamano wa malori lakini pia kuongeza mapato ya halmashauri hiyo. Anaripoti Ibrahim Yassin…(endelea).
Hayo yamebainishwa leo tarehe 8 Julai 2023 na Afisa mipango wa mji Tunduma, Broun Garigo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri kuhusu ujenzi wa mradi huo.
Amesema baada ya ujemzi wa mradi huo, imewezesha kuwa chanzo kipya cha makusanyo ya mapato ya halmashauri hiyo ambayo kwa mwezi hukusanya Sh 5.9 milioni na kwa mwaka ikiwa ni Sh 70.8 milioni.
Amesema Tunduma ni mji wa kibiashara na asilimia 75 ya bidhaa zinazovuka kutoka bandari ya Dar es salaam husafirishwa kwa malori hadi kuelekea mpaka.
Amesema mchakato wa ujenzi wa mradi huo ulianza mwaka 2021 na sasa umekamilika na kuanza kufanya kazi.
“Ni moja ya vyanzo 35 vya mapato vinavyoiwezesha Tunduma kukusanya zaidi ya Sh 11 bilioni kwa mwaka na kushika namba mbili kitaifa kwa makusanyo.
Leave a comment