JUMLA ya kesi 72 za makosa ya usafirishaji haramu wa binadamu zilifunguliwa mkoani Songwe huku watuhumiwa 127 wakihukumiwa baada ya kukutwa na hatia kutokana na biashara hiyo haramu. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).
Aidha, jumla ya wahanga 892 waliokolewa katika usafirishaji huo haramu ambapo watanzania wengi huenda kutumikishwa nje ya nchini kwa kupitia nchi mbalimbali za mipakani.
Akizungumza na MwanaHALISI Online leo tarej 8 Julai 2023 Katibu Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na usafirishaji haramu wa Binadamu kutoka Wizara ya mambo ya ndani ya nchi, Separatus Fella amesema watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti kutokana na ushirikiano mzuri wanaoupata kutoka kwa jamii ya Watanzania pamoja na vyombo vya dola.
Aidha, Mkurugenzi wa Miradi kutoka Shirika la Tanzania Relief Initiatives (TRI), Damiani Edward amesema wametoa mafunzo katika mikoa 19 Tanzania Bara na Visiwani ili kukabiliana na biashara hiyo haramu.
Amesema tayari watekelezaji 2000 wa sheria wakiwamo maofisa wa polisi, ustawi wa jamii na wadau wengine, wamepatiwa mafunzo licha ya uwepo wa uelewa mdogo katika kufanikisha hili.
Leave a comment