Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko RPC ataja chanzo ajali Songwe, majina 6 waliofariki
Habari Mchanganyiko

RPC ataja chanzo ajali Songwe, majina 6 waliofariki

Spread the love

AJALI mbaya ya gari imetokea leo  Jumatano katika barabara kuu ya Tunduma – Mbeya (TANZAM) maeneo ya Mpakani – Chapwa wilayani  Momba mkoani Songwe na kusababisha vifo vya watu sita na wengine kadhaa kujeruhiwa. Anaripoti Ibrahim Yassin,Songwe …(endelea)

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea leo tarehe 5 Julai 2023, Kamanda wa polisi mkoani Songwe, Teopista Mallya amesema ajali hiyo imetokea muda wa saa 12 .30 asubuhi.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari namba T.867 DAQ/ T.612 CXH aina ya Faw iliyokuwa ikiendeshwa na dereva ambaye amekimbia, ililigonga gari lenye namba za usajili T. 712 DXH aina ya Mitsubishi Fuso iliyokuwa ikiendeshwa na Wille Mgala.

Amesema baada ya gari hiyo aina ya Faw kuigonga Fuso, pia iliigongana Bajaji yenye namba za usajili MC 123 DUS na hatimaye gari yenye namba za usajili T.851 CZX Toyota Haice iliyokuwa ikiendeshwa na Elifaret Jackson Majera.

Amesema ajali hiyo imesababisha vifo vya watu sita papo hapo na majeruhi kadhaa ambao wamepelekwa katika Hospitali ya Tunduma.

Amewataja watu hao kuwa ni Isack Kasebele (28) mkazi wa Mwaka, Baraka Lutufyo  (23) Mkazi wa Chapwa, Fred Karagwe (28) mkazi wa Mpemba, Emmanuel Mlai  (24) mkazi wa Tunduma, John Kapizo (35) mkazi wa Majengo, na mwingine jina lake halikutambulika.

Aidha, amewataja majeruhi kuwa  ni Hassan Mwambazo (45) mkazi wa Darren es Salaam, Zainabu Hassan (43) mkazi wa Mpakani na wa tatu ni Oliver Ngusa (38) mkazi wa Chapwa.

Amesema chanzo cha ajali ni gari hiyo aina ya Faw kufeli breki na kugonga magari mengine ikiwemo Bajaji.

Amesema jitihada za kumtafuta dereva wa gari iliyosababisha ajali anatafutwa kwani ametoroka baada ya ajali hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!