Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia amrejesha Prof. Kitila Mkumbo baraza la mawaziri
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia amrejesha Prof. Kitila Mkumbo baraza la mawaziri

Spread the love

HATIMAYE Rais Samia Suluhu Hassan amemrejesha kwenye baraza lake la mawaziri, Prof. Kitila Mkumbo baada ya kukaa benchi kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja na miezi mitano. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Ikumbukwe tarehe 8 Januari 2022 Rais Samia  alifanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ambapo aliingiza mawaziri wapya na manaibu waziri huku akiwaacha baadhi ya mawaziri akiwamo Prof. Mkumbo ambaye alikuwa waziri wa uwekezaji, viwanda na biashara.

Prof. Mkumbo ambaye amekuwa mbunge kinara anayeitetea Serikali kuhusu mjadala wa mkataba uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam kupitia kampuni ya DP World ya Dubai, ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji.

Mbunge huyo wa Ubungo (CCM) ameteuliwa kushika wadhifa huo baada kutungwa kwa Sheria ya Mipango ya Taifa ya Mwaka 2023 pamoja na uamuzi wa kuhamishia masuala ya uwekezaji Ofisi ya Rais.

Taarifa iliyotolea leo tarehe 5 Julai 2023 na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, imesema Rais Samia amefanya mabadiliko madogo ya Miundo ya Wizara na kufanya uteuzi wa viongozi kama ifuatavyo: Ameunda Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji ambapo amemteua Prof. Mkumbo kuwa Waziri wa wizara hiyo.

Ameunda Wizara ya Fedha ambapo amemteua Dk. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri wa Fedha. Kabla ya uteuzi huu Mhe. Dkt. Nchemba alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Ameunda Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo amemteua, Dk. Ashatu Kachwamba Kijaji kuwa Waziri wa wizara hiyo. Kabla ya uteuzi huu, Dk. Kijaji alikuwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara.

Amemteua Lawrence Nyasebwa Mafuru kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Taifa. Kabla ya uteuzi huu Mafuru alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango (Usimamizi wa Uchumi).
Amemteua Elijah Mwandumbya kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha (Usimamizi wa Uchumi). Kabla ya uteuzi huu Mwandumbya alikuwa Kamishna, Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

error: Content is protected !!