April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ripoti ya CAG yatua bungeni

Mwita Waitara, Naibu wa Waziri wa TAMISEMI

Spread the love

RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad  imewasilishwa bungeni na  Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mwita Waitara. Anaripoti Danson Kaijage…(endelea).

Waitara aliiwasilisha ripoti hiyo leo tarehe 10 Aprili 2019 bungeni jijini Dodoma. Ikiwa zimepitia siku saba tangu Prof. Assad aiwasilishe ripoti hiyo kwa Rais John Magufuli.

“ Nawasilisha mezani Ripoti Kuu ya mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)  juu ya taarifa ya fedha kwa mwaka wa fedha wa 2017/18 ya serikali za mitaa,” amesema Mwita wakati akiwasilisha ripoti hiyo.

Sambamba na ripoti hiyo, Waitara aliwasilisha bungeni taarifa ya majibu ya serikali na mpango kazi wa utekelezaji wa mapendekezo ya  CAG, kwa hesabu ya serikali za mitaa kwa mwaka ulioshia tarehe 30 Juni 2018.

 “ Pia, nawasilisha majibu ya serikali kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2016/17 na hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa mwaka wa fedha wa 2019/20,” amesema Mwita.

error: Content is protected !!