Tuesday , 27 February 2024
Home Kitengo Michezo Namrudisha Karia aongoze FAT
Michezo

Namrudisha Karia aongoze FAT

Spread the love

YANAYOFANYWA na TFF ya rais wa sasa Wellace Karia, hayakupata kufanywa hata katika tawala za miaka 30 iliyopita. Anaandika Yusuf Abood … (endelea).

Timu kuwa na viporo 11 haikuwahi kutokea hata katika uongozi wa FAT ya kina Muhidin Ahmed Ndolanga au mtangulizi wake Said Hamad Elmaamry.

Katika ubora wa teknolojia ya sasa na miundombinu yake hutegemei kuona kisingizio chochote cha timu moja kuwa nyuma kwa michezo 11.

Jumanne ya leo tarehe 9 Aprili, 2019, timu ya Simba ilipaswa kucheza na Biashara United katika mfululizo wa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Hata hivyo, TFF imeuahirisha mchezo huo na kuifanya Simba iongeze idadi ya viporo kufikia 11, Simba imeomba kuahirishiwa mchezo huo ili ijiandae na mchezo dhidi ya TP Mazembe utakaochezwa April 13 Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Huku Simba inaahirishiwa mchezo wa leo, kule Congo TP Mazembe kesho Jumatano itacheza mchezo wa Ligi kabla ya kuivaa Simba Jumamosi.

Haya yanatokea wakati Ligi ikiwa imesalia raundi tano kumalizika, ikumbukwe ratiba ya Ligi inapaswa kumalizika tarehe 26 Mei, 2019.

Inashangaza kuona baadhi ya timu zikisalia na michezo mitano lakini Simba ina michezo 16 ambayo inapaswa ichezwe katika muda huu uliobaki.

Ni Tanzania tu na tena kwa timu ya Simba tu, na zaidi ni katika utawala wa Karia tu, ndipo utaona timu inaruhusiwa isicheze mchezo wowote wa Ligi kwa siku nane wakati ikijiandaa na mchezo wa kimataifa.

Nini kitatokea?
(i). Ili Simba iweze kukamilisha michezo 16 iliyobaki nayo katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu uliobaki, itapaswa kucheza kila baada ya siku mbili, jambo ambalo haliwezekani.

(ii). Ligi haitamalizika katika kipindi kilichopangwa awali, sababu italazimika kuisubiri Simba imalize viporo vyake.

(iii). Tutegemee timu zitakazosubiri mchezo wao wa mwisho na Simba kupata adhabu, kwa kushindwa kucheza mchezo huo.

Ligi ya msimu huu haina mdhamini, timu nyingi zina matatizo ya kifedha, tumeona baadhi wachezaji wao wakikosa mishahara na kutishia kugoma, hazitaweza kuwadhibiti wachezaji kusubiri mchezo wao mmoja wa Simba.

Fikiria timu kama Biashara na wenzao wanaochungulia shimo la kushuka daraja na pengine wakati huo zitakuwa zimeshashuka daraja, zitakuwa na sababu gani za kuingia gharama za kuzuia wachezaji kambini kusubiri mchezo mmoja usiokuwa na faida yoyote kwao?

(iv). Kwa kuwa timu nyingi zitashindwa kusubiri kucheza mchezo wa mwisho na Simba, maana yake Simba itajikusanyia point za mezani na kujihakikishia ubingwa hata kabla ya michezo yake mitano ya mwisho.

Sina hakika kama hili la kuihakikishia Simba ubingwa, ndilo lilikuwa lengo la TFF, lakini kwa ratiba inayopangwa na kupanguliwa na TFF nakosaje kufikiria hivi?

Najua mashabiki wa ‘timu’ hawatanielewa, lakini mashabiki wa mpira watanielewa. Sababu huu ni msiba mkubwa katika maendeleo ya soka letu.

Kama ningeweza kurudisha siku nyuma, ningemrudisha Karia aongoze ‘enzi za zama za Mawe’ za Elmaamry na Elmaamry aongoze enzi za sasa za teknolojia iliyokua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Wizara yaahidi kuboresha, kuimarisha michezo

Spread the loveIkiwa ni saa kadhaa baada ya kumalizika kwa mashindano ya...

Habari MchanganyikoMichezo

Nje jogging yanyakua medali 20 Kili Marathon

Spread the loveTimu ya riadha ya Wizara ya Mambo ya Nje na...

Michezo

Siku ya kukusanya maokoto ni leo, usipange kukosa

Spread the love  HATIMAYE Jumamosi imefika ndugu mteja wa Meridianbet na mechi...

Michezo

Kuwa milionea na Meridianbet ni rahisi sana

Spread the love  JE, unajua kuwa leo hii ni siku nzuri kwako...

error: Content is protected !!