Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia amtumbua Mkurugenzi Sumbawanga
Habari za Siasa

Samia amtumbua Mkurugenzi Sumbawanga

Spread the love

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na utenguzi uteuzi wa Catherine Michael Mashalla, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Pia amemteua Jaji Winfrida Beatrice Korosso kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT). Jaji Korosso ni Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Katika taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus imesema Rais Samia amemteua Bibiana Joseph Kileo kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

Kabla ya uteuzi huu Kileo alikuwa Mkuu wa Mashtaka Mkoa (RPO), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Mwanza.

Amemteua Alice Edward Mtulo kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu, Mtulo alikuwa Mkurugenzi wa ldara ya Menejimenti ya Kesi na Udhibiti Ubora, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!