Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Rais Samia mgeni rasmi kilele Mei mosi Dodoma
Habari Mchanganyiko

Rais Samia mgeni rasmi kilele Mei mosi Dodoma

Spread the love

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho siku ya wafanyakazi dunian (Mei mosi) yatakayofanyika kitaifa Jijini Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma …(endelea).

Akizungumzia na waandishi wa habari leo tarehe 14 Aprili 2022 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka amesema maandalizi ya maadhimisho hayo yatakiwa tofauti na maandalizi ya miaka mingine.

Amesema kabla ya maadhimisho hayo kutakuwa na maonesho na michezo mbalimbaliitakayoshirikisha wageni zaidi ya 3000 kutoka maeneo mbalimbali.

Aidha, katika kuhanikiza maadhimisho hayo, Mtaka pia amezindua hash tag #MEIMOSI2020dodomakivingine.

Amesema wiki ya maandalizi ya Mei Mosi mwaka huu yataanza rasmi tarehe 16 Aprili hadi tarehe 30 mwaka huu ambapo kilele itakuwa tarehe 1 Mei mwaka huu.

“Katika kufikia azma ya Serikali ya kuhakikisha kila fursa inayojitokeza inachangia ujenzi wa uchumi imara, uongozi wa mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na wadau umeazimia kutumia fursa ya Mei Mosi kitaifa kuziunganisha sekta zote za kiuchumi kwa manufaa mapana.

“Pia tumepanga kuandaa maadhimisho ya kipekee, kwani ni maadhimisho ya pili kwa Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema Mtaka.

Hata hivyo, Mtaka amesema kuanzia tarehe 16 mpaka tarehe 30 mwezi huu kutakuwa na maonesho ya michezo mbalimbali ikiwemo, mpira wa miguu, Mpira wa Pete, kuvuta Namba, kufukuza kuku, drafting, bao na riadha.

Michezo hiyo itafanyikia katika Uwanja wa Jamhuri, Chuo cha St. John, Kilimani Viterani, Sheri wajenzi, Chinangali Park vijana na Mtekelezo Dodoma Central.

Katika hatua nyingine amesema kuwa tarehe 22 Aprili hadi 30 kutakuwepo na maonesho ya OSHA ambayo yatashirikisha makundi ya wajasiliamali wadogo pamoja na kati, taasisi za umma na za huduma, wafanyabiashara wa kati na wakubwa, taasisi za fedha, viwanda, vyama vya wafanyakazi, wizara na wadau wengine.

Pamoja na hayo kutakuwepo na huduma za upimaji wa VVU, uchangiji wa damu pamoja na utoaji wa chanjo ya Uviko-19.

Aidha, amesema katika maadhimisho hayo kutakuwepo na midahalo mbalimbali kupitia vyombo vya habari kuzungumzia masuala ya vyama vya wafanyakazi, waajiri na serikali pamoja na kutunuku wafanyakazi hodari ngazi ya mkoa na kufanya ziara za utalii wa miradi.

Mtaka amewataka wakazi wa jiji la Dodoma pamoja na wilaya jirani kutumia fursa ya kufanya biashara ili kujiingizia kipato.

Pia amewaonya wafanyabiashara wa nyumba za kulala wageni kutokuwa na tamaa ya kupandisha bei za vyumba vya kukala wageni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB yafadhili ziara ya mafunzo machinga, bodaboda Dar nchini Rwanda

Spread the loveBENKI ya NMB imefadhili ziara ya siku nne ya mafunzo...

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

Habari Mchanganyiko

Wadau wataka kasi iongezeke marekebisho sheria za habari

Spread the love  WADAU wa tasnia ya habari wametakiwa kuongeza juhudi katika...

Habari Mchanganyiko

TEF yawatuliza wadau wa habari marekebisho vifungu kandamizi

Spread the love  JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limewataka wadau wa habari...

error: Content is protected !!