Spread the love

WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), imetengewa bajeti ya kiasi cha Sh. 802.29 bilioni, katika mwaka wa fedha wa 2022/23, ikiwa ni ongezeko la Sh. 120.13 bilioni ikilinganishwa na bajeti ya Sh. 722.16 bilioni iliyopitishwa 2021/2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi, bungeni jijini Dodoma na Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Innocent Bashungwa, akiwasilisha makadrio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2022/23.

“Katika mwaka wa fedha 2022/23, wakala umetengewa Sh. 802.29 bilioni kutoka vyanzo mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji wa kazi za ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya barabara,” amesema Bashungwa.

Bashungwa amesema katika mwaka huo wa fedha, TARURA inatarajia kujenga barabara za lami zenye urefu wa kilomita 411.80, za changarawe (km 10,666.11), matengenezo ya barabara (km 24,015.77), madaraja na vivuko 322, pamoja na matengenezo ya barabara (km 12,542.50).

Akichanganua matumizi ya fedha hizo, Bashungwa amesema, TARURA imetengewa Sh. 257.04 bilioni, kutoka Mfuko wa Barabara kwa ajili ya kutekeleza kazi za matengenezo ya barabara, wakati kiasi cha Sh. 325.77 bilioni, kutoka tozo ya mafuta, zikiwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara za lami, changarawe na madaraja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *