Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the love

Baraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili kwa ukubwa nchini Uturuki linatarajiwa kumtunuku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, Shahada ya udaktari wa heshima katika uchumi. Anaripoti Gabriel Mushi, Ankara-Uturuki…(endelea).

Shahada hiyo inalenga kutambua uongozi wake wa kipekee ambao umeleta mageuzi makubwa ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi nchini Tanzania.

Mageuzi hayo yametajwa kuboresha ustawi wa Watanzania; na kuimarisha sifa ya Tanzania ulimwenguni; na yamekuza mahusiano ya kibiashara, kiuchumi na kisiasa kati ya Tanzania na nchi nyingine, ikiwemo Uturuki.

Hafla ya kukabidhiwa tuzo hiyo itafanyika kesho Alhamis tarehe 18 Aprili mwaka 2024, saa sita mchana, katika Chuo Kikuu cha Ankara na ikiongozwa na Prof. Necdet Ünüvar, Mkuu wa Chuo, na kushuhudiwa na Wahadhiri na wanafunzi wa Chuo hicho.

Pia, hafla hiyo itahudhuriwa na Mabalozi wa nchi za Afrika wanaowakilisha nchi zao Uturuki.

Akizungumzia tuzo hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, amesema baada ya tukio hilo, Rais Samia ataelekea katika Ikulu ya Uturuki na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan kwa mazungumzo rasmi na Dhifa ya Kitaifa.

Baadaye Rais Samia ataelekea jijini Istanbul, mji mkuu wa kibiashara wa nchi ya Uturuki, kwa ajili ya kushiriki kwenye Kongamano la kibiashara la Tanzania na Uturuki ambalo litahudhuriwa na Makamu wa Rais wa Uturuki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

error: Content is protected !!