Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amewasili nchini Uturuki kwa ziara ya kitaifa yenye lengo la kukuza uhusiano wa diplomasia ya siasa, uchumi na biashara kati ya nchi hizo mbili. Anaripoti Gabriel Mushi, Ankara – Uturuki…(endelea).
Rais Samia ambaye ameambatana na ujumbe wa wafanyabiashara zaidi ya 100 pamoja na waandishi wa habari, amewasili jijini Ankara nchini humo saa 10:00 za jioni na kupokewa na viongozi mbalimbali Serikali ya Uturuki pamoja na Tanzania.
Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, Rais Samia anafanya ziara hiyo ya siku tano (tarehe 17-21 Aprili) baada ya Rais wa Uturuki, Tayyip Erdogan kumpa mwaliko wa kutembelea nchini humo.
“Nchi ya Uturuki ni moja nchi ipo kwenye kundi la nchi 20 wanaofanya vizuri hivyo tunajua ziara hiyo itakuwa ya kimkakati nchini kwetu,” alisema Makamba.
Alisema kuwa lengo lingine la kufanya ziara hiyo ni kupata mtaji na teknolojia ambao nchi ya Uturuki wanayo , kupata masoko ya bidhaa ambayo yapo nchini humo na kupata wawekezaji kwa lengo la kuwekeza nchini.
Leave a comment