Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia awekea mkazo sera mpya ya R-Nne
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia awekea mkazo sera mpya ya R-Nne

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan ametaka mkazo zaidi uwekewe kwenye kufundisha na kueneza sera mpya ya R-Nne inayohusu upatanishi, kuvumiliana, kuishi pamoja na kujenga nchi. Anaripoti Urumasalu Kisung’uda, TUDARCo … (endelea)

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 8 Septemba, 2022, katika kilele cha sherehe za miaka 10 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi kilichopo Kunduchi jijini Dar es Salaam ambapo alisisitiza kufundishwa kwa sera hiyo chuoni hapo ili kila mtanzania ashiriki kujenga Taifa lake.

“Hizi R nne zinahitaji kufahamika kwa undani zaidi na niombe chuo (Chuio cha Taifa cha Ulinzi) kinisaidie katika kulifundisha hilo ili kulinda usalama na kufanya nchi yetu kuwa na maendeleo.

“Watu wafundishwe kwa undani vinginevyo itabaki kuwa sera ya rais lakini tunataka kila mtu aelewe hizi watanzania waelewe kwa undani ili tuende kwa umoja kama Taifa.

Amesema Serikali imefungua nchi “uwekezaji unakua, biashara inakua, tukiendelea na ile michaka michaka yetu basi haya mengine ambayo tunayaona kwa mbele hatutayafikia.”

Asema baada ya uchaguzi ni wakati wa kila mwananchi kushiriki kujenga Taifa lake bila kujali ni nani, ili kuleta maendeleo ya pamoja badala ya mchaka mchaka wa kudai mambo mengine.

Amesema hilo linafanyika katika nchi zingine tofauti na hapa nchini ambapo amesema baada ya uchaguzi watu huanza mchakamchaka wa kudai mambo mengine.

“Mataifa mengine tukimaliza ushindani wa kisiasa, tukimaliza uchaguzi kinachoendelea ni watu kujenga taifa lao, hawachagui nani ni nani kila mwananchi kila mwenye uwezo wa huko kwa wenzetu anaingia kujenga nchi yake, sisi tukimaliza tunadai sasa mchakamcha tuendelee kudai jambo la miaka mitano ijayo tunalidai baada ya uchaguzi,” amesema Rais Samia.

Aidha ametoa rai kwa viongozi wa vyombo vya ulinzi, wizara na taasisi mbalimbali kuwateua washiriki wenye sifa kupeleka vijana katika chuo hicho pamoja na viongozi wanawake.

“Nilishiriki kutoa vyeti hapa… na nilikuta wanawake ndiyo wanaongoza kwa kufanya vizuri katika masomo.”

Amesema inafurahisha kusikia watu wengi kutoka nchi kama zaidi ya 15 wameshiriki mafunzo katika chuo hicho tangu kuanzishwa kwake mwaka 2012.

“Wale wanaosoma hapa wakirudi wakiulizwa wakisema wamesoma Tanzania tutapata watu wengi zaidi na naona baadae tutapata wengi zaidi,”

Kuhusu Chuo cha kivita ambacho awali alielezwa kuwa kipo lakini hakionekani Rais Samia alisema Serikali itakapokuwa vizuri kiuchumi itajenga mji wa medani za vita, “ili muwe vizuri kwenye medani.”

Amesema sababu ya kufanya hivyo ni Tanzania kutegemewa katika kulinda amani za nchi zingine.

Amesema sasa hivi duniani kuna vita vya aiana tatu ikiwemo ya medani, TEHAMA na uchumi na kutaka vyote kufundishwa.

Amesema pamoja na mafanikio yapo mambo anayotaka kuona yanatimia katika muda mfupi ikiwemo kwenda kufundisha ngazi za chini za wilaya na mikoa.

“Mafunzo ya huku lazima yashuke kule wanaoshika nafasi kule waelewe Tanzania inaelekea wapi na kwa maana hiyo niwatie shime chuo kijielekeze sasa kwenye kutoa kozi hizo na kama kutatakiwa msaada tutashirikiana nanyi,” amesema.

Amesema lengo la kutaka mafunzo ngazi za chini ni kuwa na wazalendo ambao wapo tayari kujenga nchi yao.

Pia alisema hivi sasa Serikali inafanya kazi ya kuwezesha wananchi wa chini, “inakwenda kwenye mapinduzi ya kilimo inakwenda kwenye kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja kule chini sasa wanaotumikia hayo lazima wawe na upeo. Tunaomba sana mtusaidie na nitafurahi likianza kwa muda mfupi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!