May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia awavunja mbavu wabunge Kenya

Spread the love

 

MABUNGE ya Kenya leo Jumatano, tarehe 5 Mei 2021, yametawaliwa na vicheko, furaha wakati Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akihutubia. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akihutubia Bunge hilo, lililojumuisha Bunge la Taifa pamoja na Bunge la Senate la Kenya, alipofika kipengele kuhusu lafudhi ya lugha ya Kiswahili, inayotumika katika bunge hilo, alisema lahaja ya Kiswahili cha Kenya ina kionjo cha pekee.

Rais Samia: Mimi binafsi huwa napenda kusikiliza Bunge la Kenya, tunafanya hivyo kwa kuwa yanayojadiliwa humo, nasi yanatuhusu. Niseme tu Bunge la Seneti la Kenya na Bunge la Taifa la Kenya linatusisimua kwa mengi.

Rais Samia: Linasimamia upana wa demokrasia yake, uzito wa mijadala yake na hamasa ya wabunge wake, tulifurahishwa zaidi na uamuzi wengi wa kuanza kutumia Kiswahili ndani Bunge.

 

Rais Samia: …na ndicho kinachonifanya nisikilize Bunge la Kenya, na-enjoy (nafurahia) kile Kiswahili kile.” Wabunge wakaangua kicheko.

Rais Samia: Kiswahili chenu kina vionjo vingi, kina vionjo vyake. Wabunge wakaangua kicheko.

Baada ya sekunde chache kupisha kicheko, Rais Samia akaendele “kionjo ambacho, chenyewe peke yake ni burudani kukisikiliza,” Bunge likazizima kwa kicheko tena.

Rais Samia: Nilikuwa namsikiliza mheshimiwa spika alivyokuwa akishindwa kutaja namba za miaka kwa Kiswahili. Kicheko kikavuma ndani ya Bunge.

Rais Samia akaendelea “…lakini inafurahisha kwamba mmeishatunga kanuni za bunge kwa kiswahili.”

Rais Samia, alikuwa nchini Kenya kwa ziara ya siku mbili, aliyoianza jana Jumanne, kwa mwaliko rasmi wa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

error: Content is protected !!