June 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Carlinho hati hati mchezo wa Simba na Yanga, Kisinda arejea

Spread the love

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga C,arlos Carlinho yupo hatihati kuukosa mchezo dhidi ya Simba, kutokana na kuumia kwenye mchezo uliopita wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Tanzania Prisons, katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaan … (endelea) 

Mchezo huo utachezwa siku ya Jumamosi tarehe 8 Mei, 2021 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akitoa taarifa za majeruhi wa timu hiyo kuelekea mchezo wa Jumamos Afisa Habari na mhamasishaji wa klabu ya Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa Carlinho anaendelea na matibabu baada ya kuumia kwenye mchezo dhidi ya Prisons na winga wao Tuisila Kisinda amerejea mara baada ya kukosekana kwenye mchezo uliopita.

Kama Carlinho atakosekana kwenye mchezo huo itakuwa ni mara yake ya tatu kuwa katika majeruhi pale unapokalibia mtanange wa watani wa jadi.

Carlinho alikosa mechi ya mzunguko wa kwanza iliyopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ambayo ilimalizika kwa sare ya bao 1-1, na mchezo wa pili ulikuwa ulikuwa visiwani Zanzibar kwenye Fainali ya Kombe la Mapinduzi ambao Yanga waliibuka na ushindi wa penalti 6-5 mara ya kutoka bila kufungana ndani ya dakiak 90.

Kurejea kwa Kisinda aliyeumia bega kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Biashara ambao Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 3-1, imerejesha matumaini kwa mashabiki wa klabu hiyo mara baada ya kufanya vizuri kwenye mchezo uliopita dhidi ya Simba.

Mchezaji huyo anarejea mara baada ya kukosekana kwenye michezo miwili mmoja ukiwa wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC, ambao Yanga walipoteza kwa bao 1-0, na mchezo dhidi ya Prisons.

error: Content is protected !!