Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Tangulizi Rais Samia awa mbogo, atumbua vigogo bandari, shirika la meli
Tangulizi

Rais Samia awa mbogo, atumbua vigogo bandari, shirika la meli

Spread the love

 

MOTO umewaka ndani ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) pamoja na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kuzivunja bodi ya taasisi hizo kwa kuwaondoa wenyeviti wake baada ya kubaini ubadhirifu wa kutisha ndani yake. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea)

Pia, ameagiza Mkurugenzi Mkuuwa TPA, Eric Hamissi; Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Salum Hamdun kuipitia ripoti ya uchunguzi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kisha kumweleza hatua watakazochukua.

Juni mwaka 2020, CAG alifanya ukaguzi maalumu wa kiuchunguzi wa mfumo wa Interprise Resource Planning (IRP) unaotumika ndani ya Mamlaka ya Bandari Tanzania nna kutoa ripoti Machi mwaka huu.

Akizungumza leo Jumamosi tarehe 4 Disemba, 2021 wakati akizindua gati katika Bandari ya Dar es Salaam, Rais Samia ameeleza kusikitishwa na Watanzania ambao wameshiriki katika ubadhirifu huo.

Wenyeviti wa bodi walioondolewa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Prof. Ignas A. Rubaratuka pamoja na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Capt. Mussa.

Amesema amepitia ripoti hiyi ya uchunguzi na kuona madudu mengi yanayofanywa ndani ya mamlaka hizo.

Amesema licha ya baadhi ya ubadhirifu huo kuonyeshwa kwenye ripoti hiyo ya CAG, hadi sasa hakuna hatua zilizochukuliwa.

Rais Samia amesema ndani ya ripoti hiyo kuna fedha nyingi zilizotumika kuajiri makampuni mbalimbali ya kuanzishwa mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji mapato ambayo haikutoa tija iliyokusudiwa.

Amesema bado kuna mianya ya uvujaji wa mapato katika mamlaka kutokana na mifumo ya malipo kuchezewa na wafanyakazi.

“Mkurugenzi, waziri, Takukuru – naomba, naagiza au naamrisha, ripoti hii nendeni mkaisome kama haipo kwenye shelf zenu mimi ninayo nitakupeni, kaitazameni muangalie yaliyopendekezwa na mkague mahesabu ya serikali alafu mchukue hatu, na nasubiri kusikia hatua mlizochukua.

“Fedha nyingine imepotea watu tunachekeana tu, tunatazamana tu, nab ado waliotajwa kwenye ile ripoti wapo maofisini kwenye Mamlaka ya Bandari sasa hivi, wanatumika na wanaendeleza ubadhirifu na wizi wa mali ya umma. Nataka kazi ifanyiwe kwenye ripoti ile na nipate hatua mlizochukua tena kwa haraka,” amesema.

Akitolea mfano madudu yaliyobainishwa ndani ya ripoti hiyo, Rais Samia amesema mamlaka ya bandari bila ya kuwa na mkakati wa Tehama na bila kushirikia mamlaka ya Serikali ya Mtandao iliajiri makampuni kadhaa kuweka mifumo mbalimbali ya ukusanyaji ndani ya bandari.

“Kampuni Sof Tech Consultant Ltd. iliajiriwa kwa mkataba wa Sh milioni 694, kati ya hizo Sh milioni 600 zililipwa kwa kampuni, lakini kampuni haikumaliza kazi mkataba ukavunjwa. Kwa maana hiyo milioni 600 zimekwenda kama mfumo umeanza kutumika au lah.

“Iliajiriwa pia kampuni ya 20 Century System kwa Dola za Marekani milioni 6.6, ambapo milioni 4.6 zililipwa na mkataba kuvunjwa baadae bila kazi kukamilika.

Ikaajiriwa kampuni ya SAP East Africa Ltd. kwa dola za Marekani 433,000 pia akaajiriwa mshauri mwelekezi binafsi kwa Dola za Marekani 31,920. Pesa hizi zote zimeingizwa kwenye mifumo.

“Lakini leo mifumo ile bado haiko vizuri inachezeleka, wafanyakazi wanadanganya na mifumo ambayo haisomani na haikusanyi fedha kwa ukamilifu wake mbali na malipo hayo ripoti inasema kulikuwa na malipo ya juu kwa wakandarasi hao bila kufuata sheria za manunuzi na matumizi,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Bandari, Eric Hamissi kusimamia na kudhibiti mapato ya mamlaka hiyo kwani, mambo yote hayo yanatokea wakati Bodi ya Wakurugenzi wa Bandari ipo, lakini hakuna hatua imechukua.

Pia amenuagiza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa kushughulikia mambo hayo amweleze kama ameshindwa ili amteua mtu mwingine wa kumsaidia.

1 Comment

  • Duh!
    Naomba “Kazi Iendelee” iwe na makali ya “Hapa Kazi Tu”. Bodi hukutana kila baada ya miezi kadhaa lakini Mkurugenzi na watendaji wengine wapo pale kila siku. Uhalifu unafanyika chini ya pua ya Mkurugenzi na watendaji wake.
    Kuvunja bodi sawa, lakini tatizo ni Mkurugenzi na watendaji wote. Bodi lazima iwe na watu makini na wenye weledi wa mizigo, mapato na matumizi.
    Idara ya Ushuru na Forodha irejeshwe. Kwani uizi wa bandarini uliongezeka baada ya kuvunjwa na uunganishwa kwa Idara ya Ushuru na Forodha na hii ya Kodi ya Mapato na kuwa TRA mweupe inaficha ukweli wa mapato ya taiga.
    Mama, tia wino kwenye kalamu kazi ichapwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Walimu 5000 Songwe waililia CWT kuwanyima sare

Spread the loveZaidi ya walimu 5000 ambao ni wanachama wa Chama cha...

error: Content is protected !!