November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Msajili ailima CUF barua, yatimua wengine

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF

Spread the love

 

MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania, Jaji Francis Mutungi, amekiandikia barua Chama cha Wananchi (CUF), akikitaka kijieleze dhidi malalamiko ya wanachama wake 10, wanaopinga kuadhibiwa ikiwemo kufukuzwa ndani ya chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa, tarehe 3 Desemba 2021 na Mkurugenzi wa Habari, Unenezi na Mahusiano na Umma CUF, Mhandisi Mohammed Ngulangwa, akizungumza na wanahabari mkoani Dar es Salaam.

“Tarehe 27 Novemba mwaka huu, chama kilipokea barua kutoka kwa msajili ya tarehe 26 Novemba 2021, iliyoelekezwa kwa katibu mkuu wa chama, inayohusu kuwasilisha maelezo kuhusu malalamiko yaliyowasilishwa kwake na waliokuwa wanachama wa CUF,” amesema Mhandisi Ngulangwa.

Mkurugenzi huyo wa habari CUF, amesema Jaji Mutungi anakitaka chama hicho kijileleze dhidi ya maamuzi yaliyochukulia na vikao vya Baraza lake Kuu la Uongozi, vilivyofanyika tarehe 5 na 6, Novemba 2021.

Jaji Francis Mungi, Msajili wa Vyama vya Siasa

Ambayo yalikuwa ni hatua za kinidhamu dhidi ya wanachama wake wanaodaiwa kukiuka maadili ya CUF.

Ambapo wanachama hao wanapinga kuchukuliwa hatua hizo, wakidai ni kinyume na katiba ya chama hicho, kwani ilikiukwa wakati maamuzi hayo yanachukuliwa, ikiwemo akidi ya wajumbe wa kikao kutotimia.

Mhandisi Ngulangwa, amewataja wanachama hao waliomuandikia barua Jaji Mutungi, akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana CUF (JUVICUF),Hamidu Bobali, aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari CUF, Abdul Kambaya.

Wengine ni, Mussa Haji Kombo, Ali Makame Issa, Mtumwa Abdallah, Hamda Abdallah na Mohamed Makame.

Mhandisi Ngulangwa amesema kuwa, CUF imeshajibu malalamiko hay0.

“Baada ya kuwa tumepokea barua kutoka kwa msajili tumejibu, tunasubiri msajili atoe muongzoo kama sheria inavyomtaka ,”

“Tunaamini msajili ataongozwa vyema na maelezo yetu na katiba ya CUF toleo la 2019 yaliyofanunua walalamijika jinsi maamuzi ya baraza kuu yalivyozinagatia taratibu zote,” amesema Mhandiusi Ngulangwa.

Wakati huo huo, Mhandisi Ngulangwa amesema Kamati ya Uongozi wa Taifa ya CUF, imeuvunja uongozi wa Kamati ya Utendaji ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, ikidaiwa ilichochea mgogoro ndani ya chama hicho.

Mhandisi Mohammed Ngulangwa, Mkurugenzi wa Habari -CUF

“Kamati ya uongozi wa taifa imepewa mamlaka ya kuvunja uongozi wa kamati za utendaji za wilaya,” amesema Mhandisi Ngulangwa.

Mhandisi Ngulangwa amesema “Kwa mujibu wa Ibara ya 86 (1B) ya 2019, kwa kutumia mamlaka hayo kamati ya uongozi wa taifa imeivunja kamati ya utendaji ya Wilaya ya Kinondoni, ili kuboresha ujenzi wa chama wilayani humo.”

Viongozi wa kamati hiyo waliovuliwa nafasi zao ni, Rajab Salum (Mwenyekiti), Seleman Masauni (Kaimu Katibu) na wajumbe wengine ambao ni, Salma Majere, Juma Mahimbo, Shaaban Choga na Juma Mateleka.

Wengine ni, Mohammed Kamanyola, Pili Songa, Fatuma Magoga na Athuman Chachala.

Aidha, Mhandisi Ngulangwa, amezionya kamati tendaji za wilaya nyingine kujiepusha na migogoro ndani ya chama, ili zisichukuliwe hatua.

“Majukumu ya Kamati ya Uongozi wa Taifa, kuhakikisha Kamati za Utendaji za Wilaya zinajikita katika ujenzi na uimarishaji chama, kujiepusha kushiriki kuanzisha au kuchagiza migogoro na utovu wa nidhamu,” amesema Mhandisi Ngulangwa.

error: Content is protected !!