Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia ateua viongozi 12, kigogo CCM ateuliwa RC Shinyanga
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ateua viongozi 12, kigogo CCM ateuliwa RC Shinyanga

Spread the love

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na kuwahamisha viongozi 12, ikiwa ni siku chache tangu alivyofanya mabadiliko ya baadhi ya viongozi wa mikoa na wilaya Jumamosi ya tarehe 9 Machi 2024. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Panga pangua hiyo imetangazwa leo Jumanne na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus.

Katika mabadiliko hayo, Rais Samia ameteua Mkuu wa Mkoa mmoja, wakuu wa wilaya wawili, wakurugenzi watendaji wa halamshauri watatu,makatibu tawala wa wilaya wawili na kuwahamisha wakurugenzi watendaji wa halamshauri watatu.

Katika uteuzi huo, Rais Samia amemteua aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Anamringi Macha, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Macha anachukua nafasi ya Christina Mndeme, ambaye ameteuliwa na Rais Samia kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.

“Uapisho wa Mkuu wa mkoa na katibu Mkuu utafanyika tarehe 13 Machi 2024, Ikulu Dar es Salaam,” imesena taarifa ya Zuhura.

Kwa upande wa wakuu wa wilaya, Japhari Kubecha Mghamba, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto na  Mussa Kilakala, ameteuliwa kuwa Mkuu wa  Wilaya ya Pangani.

Rais Samia amemteua aliyekuwa Afisa Mwandamizi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,  Robert Masunya, kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Naye Mwashabani Mrope, ameteuliwa na Rais Samia kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.

Wakurugenzi Watendaji waliohamishwa ni, Frederick Dagamiko, aliyeondolewa Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwenda Halmashauri ya Jiji la Tanga. Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Bashir Muhoja, amepelekwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea.

Na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tito Mganwa, amehamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.

3 Comments

  • Of course kozi hii imekuja mda mwafaka, maana wizi umekuwa na athali kubwa kwa uchumi wa mtu mmojammoja

  • Mbona Rais anahangaika na “kuteua na kuhamisha” badala ya kusimamia waliopo madarakani walete matokeo mazuri. Inaoneka hali siyo shwari ndani ya CCM na Serikalini. Mbaya zaidi anarudia kuteua na kuhamisha watu wale wale!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!