Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia ateta na mjumbe maalum wa waziri mkuu Uingereza
Habari za Siasa

Rais Samia ateta na mjumbe maalum wa waziri mkuu Uingereza

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Mjumbe Maalum wa Boris Jonson, Waziri Mkuu wa Uingereza katika masuala ya biashara kati ya Uingereza na Tanzania, Lord John Walney. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Ni jana Jumapili, tarehe 31 Oktoba 2021, katika mji wa Glasgow, Scotland
ambapo Walney alikutana na Rais Samia kujitambulisha akiwa na jukumu la kuwa kiungo kati ya nchi hizo mbili kuhusu masuala ya biashara, uwekezaji na utalii.

Amesema, kukutana kwake na Rais Samia kumempa fursa ya kujua vipaumbele vya Serikali ya Tanzania ambavyo vitamwezesha kuwashawishio wafanyabiashara wa Uingereza kuwekeza katika sekta ya biashara na utalii nchini Tanzania.

Kwa upande wake, Rais Samia amemshukuru Walney kwa uamuzi wake wa kukutana naye na kujitambulisha kwake na kumueleza Serikali ya Tanzania ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Uingereza katika kuchochea biashara baina ya nchi mbili hizo.

Rais Samia amesema, Serikali ya Uingereza na Tanzania zimekuwa na ushirikiano wa kibiashara kwa muda mrefu ambapo Uingereza ni moja kati ya nchi zinazoongoza kuwekeza nchini Tanzania, hivyo kupitia mjumbe huyo kutaongeza fursa zaidi za kibiashara katika kukuza ushirikiano wa uchumi na Uingereza.

Taarifa ya mazungumzo hayo, imetolewa na Jaffar Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Rais Samia yupo nchini Scotland, kuhudhulia mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa unaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP26) ambapo kesho Jumanne, tarehe 2 Novemba 2021, atakuwa miongoni mwa viongozi watakaohutubia mkutano huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

error: Content is protected !!