Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia ashuhudia mikataba ya msaada wa bilioni 455
Habari za Siasa

Rais Samia ashuhudia mikataba ya msaada wa bilioni 455

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini wa mikataba mitatu ya msaada wa maendeleo inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) wenye thamani ya Euro milioni 179.35 sawa na Sh 455 bilioni. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Aidha, Rais Samia ameshuhudia kutangazwa kwa fedha za msaada wa bajeti ya Serikali zilizotolewa na EU kiasi cha Euro milioni 46.11 sawa na Sh 117.036 bilioni kwa mwaka wa fedha 2022/ 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Manfredo Fantl, wakati Balozi Fantl alipofika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma 04 Julai, 2023.

Fedha hizo zitaelekezwa katika sekta za maendeleo hasa katika uchumi wa Buluu, uwezeshaji wananchi kiuchumi pamoja na uimarishaji mifumo ya ukusanyaji na lisimamizi wa fedha serikalini.

Katika hafla hiyo iliyofanyika leo tarehe 4 Julai 2023 ukumbi wa Hazina Rais Samia ameishukuru EU kwa kuwa msaada huo ni matokeo ya ziara aliyoifanya Brussels, Ubelgiji alipokutana na Rais wa Tume ya Ulaya Mhe. Ursula Von der Leyen.

Msaada huo uliotolewa kwa Serikali unaendana na mipango mkakati ya kisekta na maendeleo nchini, hususan Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025 na Dira ya Macndeleo ya Zanzibar 2050.

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali mara baada ya Utiaji Saini wa Mikataba Mitatu ya msaada uliotolewa na Umoja wa Ulaya yenye thamani ya Euro Milioni 179.35 sawa na Sh 455.09 bilioni.

Aidha, Rais Samia amesema Programu hizo pia zitaendana na kaulimbiu ya Mwaka wa Fedha wa 2023/24, kama ilivyopitishwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC):

“Kuongeza kasi ya kufufua uchumi, kukabiliana na kupunguza mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuinarisha sekta zemye tija kwa naisha bora”.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!