Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia aondoa zuio la mikutano hadhara ya vyama vya siasa
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia aondoa zuio la mikutano hadhara ya vyama vya siasa

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan, ameondoa zuio la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, lililowekwa na mtangulizi wake, Hayati John Magufuli, kwa maelezo kwamba kuipa nafasi Serikali kufanya kazi ya kuijenga nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia ameondoa marufuku hiyo leo Jumanne, tarehe 3 Januari 2023, akizungumza na viongozi wakuu wa vyama vya siasa vya upinzani Tanzania, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Samia amesema Serikali itawakuwa na wajibu wa kulinda mikutano hiyo ili ifanyike kwa amani, huku akivitaka vyama vya siasa kutoa taarifa juu ya ratiba ya mikutano hiyo.

“Nianze na la mikutano ya hadhara, hii ni haki kwa sheria zetu. Ni haki ya vyama kufanya mikutano yao ya hadhara na kwa bahati taarifa zote mbili zimeibuka kama ni jambo muhimu sana. Uwepo wangu leo mbele yenu ni kuja kutoa ruhusa, kuja kutangaza kwamba lile tangazo la kuzuia mikutano ya hadhara sasa linaondolewa,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amevitaka vyama hivyo kufanya mikutano ya hadhara kwa kuzingatia sheria za nchi, pamoja na kufanya siasa za kistaarabu na zenye kuibua hoja zitakazoleta maendeleo ya Taifa.

“Wajibu wenu vyama ni kufuata sheria zinavyosema, ni kufuata kanuni zinavyosema ndiyo wajibu wenu. Lakini kama waungwana wastaarabu niwaombe sana, tunatoa ruhusa ya vyama vya siasa twendeni tukafanye siasa za kistaarabu, za kupevuka. Tukafanye siasa za kujenga na si kubomo, kurudi nyuma,” amesema Rais Samia.

Katika hatua nyingine, Rais Samia amesema Serikali yake na Chama chake cha Mapinduzi (CCM), ni muumini wa kukubali kukosolewa kwa kuwa inapata nafasi ya kujua changamoto zilizopo kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!